Judges 19:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo Mlawi na suria wake pamoja na mtumishi wake walipoinuka kwenda zao, baba mkwe wake akamwambia huyo Mlawi, “Sasa mchana umekwisha na jioni imekaribia. Ulale hapa, na kufurahi. Kesho asubuhi utaamka mapema kuanza safari yako ya kurudi nyumbani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha yule mtu alipoinuka aende zake pamoja na suria wake na mtumishi wake, baba mkwe wake, yaani baba wa yule msichana, akamwambia, “Tazama sasa jioni inakaribia. Ulale hapa, usiku unakaribia. Ukae, ukajifurahishe nafsi yako. Kesho unaweza kuamka asubuhi na mapema uende nyumbani kwako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha hapo mtu huyo alipoinuka ili aende zake, yeye na suria yake, na mtumishi wake, huyo mkwewe, baba yake mwanamke, akamwambia, Tazama mchana wakaribia jioni, tafadhali kaa usiku kucha; tazama mchana wakaribia mwisho wake, lala hapa, ili moyo wako ufurahi; hata kesho uende zako asubuhi na mapema, ili upate kwenda kwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo Mlawi na suria wake pamoja na mtumishi wake walipoinuka kwenda zao, baba mkwe wake akamwambia huyo Mlawi, “Sasa mchana umekwisha na jioni imekaribia. Ulale hapa, na kufurahi. Kesho asubuhi utaamka mapema kuanza safari yako ya kurudi nyumbani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi wakati yule mtu alipoinuka aende zake, pamoja na suria wake na mtumishi wake, baba mkwe wake, yaani, baba wa yule msichana akamwambia, “Tazama sasa jioni inakaribia. Ulale hapa usiku unakaribia. Ukae, ukajifurahishe nafsi yako. Kesho unaweza kuamka mapema asubuhi na uende nyumbani kwako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi wakati yule mtu alipoinuka aende zake, pamoja na suria wake na mtumishi wake, baba mkwe wake, yaani, baba wa yule msichana akamwambia, “Tazama sasa jioni inakaribia. Ulale hapa usiku unakaribia. Ukae, ukajifurahishe nafsi yako. Kesho unaweza kuamka mapema asubuhi na uende nyumbani kwako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha hapo mtu huyo alipoinuka ili aende zake, yeye na suria wake, na mtumishi wake, huyo mkwewe, baba yake mwanamke, akamwambia, Tazama mchana wakaribia jioni, tafadhali kaa usiku kucha; tazama mchana wakaribia mwisho wake, lala hapa, ili moyo wako ufurahi; hata kesho uende zako asubuhi na mapema, ili upate kwenda kwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo Mlawi na suria wake pamoja na mtumishi wake walipoinuka kwenda zao, baba mkwe wake akamwambia huyo Mlawi, “Sasa mchana umekwisha na jioni imekaribia. Ulale hapa, na kufurahi. Kesho asubuhi utaamka mapema kuanza safari yako ya kurudi nyumbani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule mtu alipoondoka, aende zake, yeye na suria yake na mtumishi wake, mkwewe, babake yule kijana wa kike, akamwambia: Tazama, mchana umekwisha fikia kuwa jioni, afadhali ulale! Tazama, jua limekwisha kuchwa; lala hapa, moyo wako upate kuchangamka! Kesho mtajidamka kwenda zenu, ufike hemani kwako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha hapo mtu huyo alipoinuka ili aende zake, yeye na suria yake, na mtumishi wake, huyo mkwewe, baba yake mwanamke, akamwambia, Tazama mchana wakaribia jioni, tafadhali kaa usiku kucha; tazama mchana wakaribia mwisho wake, lala hapa, ili moyo wako ufurahi; hata kesho uende zako asubuhi na mapema, ili upate kwenda kwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule Mulawi na habara yake pamoja na mutumishi wake waliposimama kwenda zao, baba mukwe wake akamwambia yule Mulawi: “Sasa muchana umekwisha na magaribi imekaribia. Ulale hapa, na kufurahi. Kesho asubui utaamuka mapema kuanza safari yako ya kurudi kwako.”