Judges 2:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, hasira ya Mwenyezi-Mungu iliwaka dhidi ya Israeli, naye akawaacha wanyanganyi wapore mali zao. Aliwakabidhi kwa adui zao waliowazunguka hata wasiweze tena kuwapinga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo hasira ya Mwenyezi Mungu ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, hasira ya Mwenyezi-Mungu iliwaka dhidi ya Israeli, naye akawaacha wanyang'anyi wapore mali zao. Aliwakabidhi kwa adui zao waliowazunguka hata wasiweze tena kuwapinga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo hasira ya bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, hasira ya Mwenyezi-Mungu iliwaka dhidi ya Israeli, naye akawaacha wanyanganyi wapore mali zao. Aliwakabidhi kwa adui zao waliowazunguka hata wasiweze tena kuwapinga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo makali ya Bwana yakawawakia waisiraeli, akawatia mikononi mwa wanyang'anyi, wawanyang'anye mali zao, namo mikononi mwa adui zao waliowazunguka, akawauza, wasiweze tena kusimama usoni pao adui zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, hasira ya Yawe ikawaka juu ya Israeli, naye akawaacha wanyanganyi wanyanganye mali zao. Akawatoa kwa waadui zao waliowazunguka hata wasiweze tena kuwashinda.