Judges 2:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila walipokwenda kupigana, mkono wa Mwenyezi-Mungu uliwakabili kuwaletea balaa, kama alivyokuwa amewaonya na kuapa. Nao wakawa katika huzuni kubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wowote Israeli walipotoka kwenda kupigana, mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa kinyume nao ili awashinde, kama vile alivyokuwa amewaapia. Nao wakawa katika taabu kubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila walipokwenda kupigana, mkono wa Mwenyezi-Mungu uliwakabili kuwaletea balaa, kama alivyokuwa amewaonya na kuapa. Nao wakawa katika huzuni kubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Po pote Israeli walipotoka kwenda kupigana, mkono wa BWANA ulikuwa kinyume nao ili kuwashinda, kama vile alivyokuwa amewaapia. Nao wakawa katika taabu kubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Popote Israeli walipotoka kwenda kupigana, mkono wa bwana ulikuwa kinyume nao ili kuwashinda, kama vile alivyokuwa amewaapia. Nao wakawa katika taabu kubwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila walikokwenda mkono wa BWANA ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama BWANA alivyosema, na kama BWANA alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila walipokwenda kupigana, mkono wa Mwenyezi-Mungu uliwakabili kuwaletea balaa, kama alivyokuwa amewaonya na kuapa. Nao wakawa katika huzuni kubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Po pote walipotokea, mkono wa Bwana ukawapatia mabaya, kama Bwana alivyowaambia, kama Bwana alivyowaapia; kwa hiyo wakasongeka sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila walikokwenda mkono wa BWANA ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama BWANA alivyosema, na kama BWANA alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mara walipokwenda kupigana, mukono wa Yawe ulipambana nao kwa kuwaletea hasara, kama alivyokuwa amewaonya na kuapa. Nao wakakuwa katika huzuni kubwa.