Judges 2:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mara Mwenyezi-Mungu alipowapelekea mwamuzi, yeye mwenyewe alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa mikononi mwa adui zao muda wote wa uhai wa mwamuzi huyo. Aghalabu, Mwenyezi-Mungu aliwaonea huruma aliposikia kilio chao kutokana na mateso na dhuluma walizofanyiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mara Mwenyezi Mungu alipowainulia mwamuzi, Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja na huyo mwamuzi, naye aliwaokoa kutoka mikononi mwa adui zao kwa kipindi chote alichoishi yule mwamuzi. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwahurumia kwa sababu ya kilio chao cha huzuni kwa ajili ya wale waliokuwa wakiwatesa na kuwataabisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wakati Bwana alipowainulia waamuzi, ndipo Bwana alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana Bwana alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mara Mwenyezi-Mungu alipowapelekea mwamuzi, yeye mwenyewe alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa mikononi mwa adui zao muda wote wa uhai wa mwamuzi huyo. Aghalabu, Mwenyezi-Mungu aliwaonea huruma aliposikia kilio chao kutokana na mateso na dhuluma walizofanyiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mara BWANA alipowainulia mwamuzi, BWANA alikuwa pamoja na huyo mwamuzi, naye aliwaokoa kutoka mikononi mwa adui zao kwa kipindi chote alichoishi yule mwamuzi. Kwa kuwa BWANA aliwahurumia kwa sababu ya kilio chao cha huzuni kwa ajili ya wale waliokuwa wakiwatesa na kuwataabisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mara bwana alipowainulia mwamuzi, bwana alikuwa pamoja na huyo mwamuzi, naye aliwaokoa kutoka mikononi mwa adui zao kwa kipindi chote alichoishi yule mwamuzi. Kwa kuwa bwana aliwahurumia kwa sababu ya kilio chao cha huzuni kwa ajili ya wale waliokuwa wakiwatesa na kuwataabisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kila wakati BWANA alipowainulia waamuzi, ndipo BWANA alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana BWANA alisikitishwa na kilio chao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mara Mwenyezi-Mungu alipowapelekea mwamuzi, yeye mwenyewe alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa mikononi mwa adui zao muda wote wa uhai wa mwamuzi huyo. Aghalabu, Mwenyezi-Mungu aliwaonea huruma aliposikia kilio chao kutokana na mateso na dhuluma walizofanyiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana alipowainulia waamuzi, Bwana alikuwa na yule mwamuzi, awaokoe mikononi mwa adui zao siku zote za huyu mwamuzi, kwani Bwana aliwaonea uchugu, walipompigia kite kwa ajili yao waliowatesa na kuwasukumasukuma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wakati BWANA alipowainulia waamuzi, ndipo BWANA alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana BWANA alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mara Yawe alipowapelekea mwamuzi, yeye mwenyewe alikuwa pamoja na mwamuzi yule, akawaokoa toka katika mikono ya waadui zao muda wote wa maisha ya mwamuzi yule. Ingawa hivyo, Yawe aliwaonea huruma aliposikia kilio chao kutokana na mateso na masumbuko yao.