Judges 20:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa kabila la Benyamini walikusanya kutoka miji yao jeshi la watu 26,000 wenye kutumia silaha, nao wakazi wa mji wa Gibea wakakusanya watu 700 waliochaguliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ile Wabenyamini wakakusanya watu elfu ishirini na sita kutoka miji yao waliojifunga panga, mbali na hao vijana wenye uwezo mia saba kutoka wale walioishi Gibea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao wana wa Benyamini walihesabiwa siku ile kutoka hiyo miji, watu waume ishirini na sita elfu waliotumia upanga, zaidi ya hao waliokaa Gibea, ambao walihesabiwa watu wateule mia saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa kabila la Benyamini walikusanya kutoka miji yao jeshi la watu 26,000 wenye kutumia silaha, nao wakazi wa mji wa Gibea wakakusanya watu 700 waliochaguliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ile Wabenyamini wakakusanya watu 26,000 kutoka katika miji yao, waliojifunga panga, mbali na hao 700 waliochaguliwa miongoni mwa hao waliokaa Gibea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ile Wabenyamini wakakusanya watu 26,000 kutoka miji yao, waliojifunga panga, mbali na hao 700 waliochaguliwa miongoni mwa hao waliokaa Gibea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao wana wa Benyamini walihesabiwa siku ile kutoka hiyo miji, wanaume elfu ishirini na sita waliokuwa na silaha, mbali na hao waliokaa Gibea, ambao walihesabiwa watu wateule mia saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa kabila la Benyamini walikusanya kutoka miji yao jeshi la watu 26,000 wenye kutumia silaha, nao wakazi wa mji wa Gibea wakakusanya watu 700 waliochaguliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Benyamini waliotoka mijini walipojikagua siku hiyo wlikuwa watu 26000 waliojua kuchomoa panga pasipo wenyeji wa Gibea waliokaguliwa kuwa watu wateule 700.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao wana wa Benyamini walihesabiwa siku ile kutoka hiyo miji, watu waume ishirini na sita elfu waliotumia upanga, zaidi ya hao waliokaa Gibea, ambao walihesabiwa watu wateule mia saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa kabila la Benjamina wakakusanya kutokea miji yao jeshi la watu elfu makumi mbili na sita wenye kutumia silaha, nao wakaaji wa muji wa Gibea wakakusanya watu mia saba waliochaguliwa.