Judges 20:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kati ya watu hao waliochaguliwa kulikuwa na watu 700 waliotumia mkono wa kushoto; kila mmoja aliweza kurusha jiwe kwa kombeo na kulenga unywele bila kukosea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miongoni mwa askari hao, palikuwa na askari mia saba waliochaguliwa waliotumia mkono wa kushoto; kila mmoja wao angetupa jiwe kwa kombeo na kulenga unywele bila kukosa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika watu hao wote walikuwako watu waume mia saba waliochaguliwa, wenye shoto; kila mmoja alikuwa anaweza kuutupia unywele mawe kwa teo, wala asikose.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kati ya watu hao waliochaguliwa kulikuwa na watu 700 waliotumia mkono wa kushoto; kila mmoja aliweza kurusha jiwe kwa kombeo na kulenga unywele bila kukosea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miongoni mwa hao askari wote kulikuwa na watu 700 bora waliochaguliwa watumiao mkono wa kushoto, kila mmoja wao aliweza kutupa jiwe kwa kombeo na kulenga unywele mmoja bila kukosa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miongoni mwa hao askari wote kulikuwa na watu 700 bora waliochaguliwa watumiao mkono wa kushoto, kila mmoja wao aliweza kutupa jiwe kwa kombeo na kulenga unywele mmoja bila kukosa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika watu hao wote walikuwako wanaume mia saba waliochaguliwa, wenye shoto; kila mmoja alikuwa anaweza kuutupia unywele mawe kwa kombeo, wala asikose.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kati ya watu hao waliochaguliwa kulikuwa na watu 700 waliotumia mkono wa kushoto; kila mmoja aliweza kurusha jiwe kwa kombeo na kulenga unywele bila kukosea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika watu hawa wote walikuwa watu 700 waliochaguliwa kwa kuwa wenye shoto; kila mmoja wao alijua kutupa mawe kwa kombeo, asikose, ijapo uwe unywele tu, aliotaka kuupiga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika watu hao wote walikuwako watu waume mia saba waliochaguliwa, wenye shoto; kila mmoja alikuwa anaweza kuutupia unywele mawe kwa teo, wala asikose.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kati ya watu hao waliochaguliwa kulikuwa watu mia saba waliotumia zaidi mukono wa kushoto; kila mumoja aliweza kurusha jiwe kwa mujeledi na kupiga unywele bila kukosa.