Judges 20:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli wakaenda Betheli kutaka shauri kwa Mungu, wapate kujua kabila ambalo litakwenda kwanza kupigana na watu wa kabila la Benyamini. Mwenyezi-Mungu alitaja kabila la Yuda liende kwanza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli wakapanda Betheli na kumuuliza Mungu, “Ni nani miongoni mwetu atakayetangulia mbele yetu ili kupigana na Wabenyamini?” Mwenyezi Mungu akawajibu, “Yuda ndiye atakayetangulia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wana wa Israeli wakainuka, wakakwea kwenda Betheli, nao wakataka shauri kwa Mungu; wakasema, Ni nani atakayekwea kwenda vitani kwanza kwa ajili yetu juu ya wana wa Benyamini? Bwana akawaambia, Yuda atakwea kwanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli wakaenda Betheli kutaka shauri kwa Mungu, wapate kujua kabila ambalo litakwenda kwanza kupigana na watu wa kabila la Benyamini. Mwenyezi-Mungu alitaja kabila la Yuda liende kwanza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli wakapanda Betheli na kumwuliza Mungu, “Ni nani miongoni mwetu atakayetangulia mbele yetu ili kupigana na Wabenyamini?” BWANA akawajibu, “Yuda ndiye atakayetangulia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli wakapanda Betheli na kumuuliza Mungu, “Ni nani miongoni mwetu atakayetangulia mbele yetu ili kupigana na Wabenyamini?” bwana akawajibu, “Yuda ndiye atakayetangulia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wana wa Israeli wakainuka, wakakwea kwenda Betheli, nao wakataka shauri kwa Mungu; wakasema, Ni nani atakayekwea kwenda vitani kwanza kwa ajili yetu juu ya wana wa Benyamini? BWANA akawaambia, Yuda atakwea kwanza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli wakaenda Betheli kutaka shauri kwa Mungu, wapate kujua kabila ambalo litakwenda kwanza kupigana na watu wa kabila la Benyamini. Mwenyezi-Mungu alitaja kabila la Yuda liende kwanza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Waisiraeli wakaondoka, wakapanda kwenda Beteli, wakamwuliza Mungu, wana wa Isiraeli wakisema: Ni wa nani wa kwetu, ndio waanze kupigana na wana wa Benyamini? Bwana akasema: Wayuda na waanze!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wana wa Israeli wakainuka, wakakwea kwenda Betheli, nao wakataka shauri kwa Mungu; wakasema, Ni nani atakayekwea kwenda vitani kwanza kwa ajili yetu juu ya wana wa Benyamini? BWANA akawaambia, Yuda atakwea kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli wakaenda Beteli kuomba shauri kwa Mungu, wapate kujua kabila ambalo litakwenda kwanza kupigana na watu wa kabila la Benjamina. Yawe akataja kabila la Yuda liende kwanza.