Judges 20:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Viongozi wote wa makabila ya Israeli wakajitokeza mbele ya mkusanyiko wa watu wa Mungu. Wote, jumla walikuwa askari wa miguu wenye silaha 400,000.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Viongozi wote wa makabila ya Israeli wakakaa kwenye nafasi zao katika kusanyiko la watu wa Mungu, ambao walikuwa askari elfu mia nne walioenda kwa miguu wenye panga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao wakuu wa watu, maana wakuu wa kabila zote za Israeli, wakajihudhurisha katika huo mkutano wa watu wa Mungu, watu waume mia nne elfu waendao kwa miguu, wenye kutumia upanga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Viongozi wote wa makabila ya Israeli wakajitokeza mbele ya mkusanyiko wa watu wa Mungu. Wote, jumla walikuwa askari wa miguu wenye silaha 400,000.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Viongozi wote wa kabila za Israeli wakakaa kwenye nafasi zao katika kusanyiko la watu wa Mungu, askari 400,000 waendao kwa miguu wenye panga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Viongozi wote wa kabila za Israeli wakakaa kwenye nafasi zao katika kusanyiko la watu wa Mungu, askari 400,000 waendao kwa miguu wenye panga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakuu wote wa makabila yote ya Israeli, wakahudhuria huo mkutano wa watu wa Mungu, wanaume elfu mia nne waendao kwa miguu, walio na silaha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Viongozi wote wa makabila ya Israeli wakajitokeza mbele ya mkusanyiko wa watu wa Mungu. Wote, jumla walikuwa askari wa miguu wenye silaha 400,000.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wote waliokuwa pembeni kwa watu wa mashina yote ya Waisiraeli wakatokea katika mkutano wao walio ukoo wa Mungu, watu 400000 waliokwenda kwa miguu waliojua kuchomoa panga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao wakuu wa watu, maana wakuu wa kabila zote za Israeli, wakajihudhurisha katika huo mkutano wa watu wa Mungu, watu waume mia nne elfu waendao kwa miguu, wenye kutumia upanga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Viongozi wote wa makabila ya Israeli wakajitokeza mbele ya mukusanyiko wa watu wa Mungu. Wote kwa jumla walikuwa waaskari elfu mia ine wa miguu wenye silaha.