Judges 20:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi Waisraeli wakaenda juu, wakamlilia Mwenyezi-Mungu mpaka jioni. Kisha wakaomba shauri kwa Mwenyezi-Mungu: “Je, twende tena kupigana na ndugu zetu, wa kabila la Benyamini?” Mwenyezi-Mungu akawajibu, “Nendeni mkapigane nao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli wakapanda mbele za Mwenyezi Mungu na kulia mbele zake hadi jioni. Nao wakamuuliza Mwenyezi Mungu, “Je, tupande tena kupigana vita na Wabenyamini, ndugu zetu?” Mwenyezi Mungu akajibu, “Pandeni mkapigane nao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wa Israeli wakakwea juu na kulia mbele za Bwana hata jioni; wakamwuliza Bwana, wakisema, Je! Niende nikaribie tena kupiga vita juu ya wana wa Benyamini ndugu yangu? Bwana akasema, Haya, kweeni, mwende kupigana naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi Waisraeli wakaenda juu, wakamlilia Mwenyezi-Mungu mpaka jioni. Kisha wakaomba shauri kwa Mwenyezi-Mungu: “Je, twende tena kupigana na ndugu zetu, wa kabila la Benyamini?” Mwenyezi-Mungu akawajibu, “Nendeni mkapigane nao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli wakapanda mbele za BWANA na kulia mbele zake mpaka jioni, nao wakamwuliza BWANA wakisema, “Je, tupande tena kupigana vita na Wabenyamini, ndugu zetu?” BWANA akajibu, “Pandeni mkapigane nao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli wakapanda mbele za bwana na kulia mbele zake mpaka jioni, nao wakamuuliza bwana wakisema, “Je, tupande tena kupigana vita na Wabenyamini, ndugu zetu?” bwana akajibu, “Pandeni mkapigane nao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wana wa Israeli wakakwea juu na kulia mbele za BWANA hadi jioni; wakamwuliza BWANA, wakisema, Je! Niende nikaribie tena kupiga vita juu ya wana wa Benyamini ndugu yangu? BWANA akasema, Haya, kweeni, mwende kupigana naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi Waisraeli wakaenda juu, wakamlilia Mwenyezi-Mungu mpaka jioni. Kisha wakaomba shauri kwa Mwenyezi-Mungu: “Je, twende tena kupigana na ndugu zetu, wa kabila la Benyamini?” Mwenyezi-Mungu akawajibu, “Nendeni mkapigane nao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini tena walikuwako wana wa Isiraeli waliopanda na kumlilia Bwana mchana kutwa, wakamwuliza Bwana kwamba: Tuendelee kujisogeza, tupigane na wana wa Benyamini walio ndugu zetu? Bwana akawaambia: Haya! Wapandieni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wa Israeli wakakwea juu na kulia mbele za BWANA hata jioni; wakamwuliza BWANA, wakisema, Je! Niende nikaribie tena kupiga vita juu ya wana wa Benyamini ndugu yangu? BWANA akasema, Haya, kweeni, mwende kupigana naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Waisraeli wakaenda juu, wakamulilia Yawe mpaka magaribi. Kisha wakaomba shauri kwa Yawe: “Twende tena kupigana na wandugu zetu, wa kabila la Benjamina?” Yawe akawajibu: “Muende mupigane nao.”