Judges 20:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote wa jeshi la Waisraeli wakaenda Betheli. Walikaa huko mbele ya Mwenyezi-Mungu wakiomboleza na kufunga mpaka jioni. Wakamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo jeshi lote, na Waisraeli wote, wakapanda Betheli, na huko wakakaa mbele za Mwenyezi Mungu wakilia. Wakafunga siku hiyo hadi jioni na kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo wana Israeli wote, na hao watu wote, wakakwea, wakaenda Betheli, na kulia, wakaketi hapo mbele za Bwana, wakafunga siku hiyo hata jioni; nao wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote wa jeshi la Waisraeli wakaenda Betheli. Walikaa huko mbele ya Mwenyezi-Mungu wakiomboleza na kufunga mpaka jioni. Wakamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Waisraeli, watu wote, wakapanda Betheli, huko wakakaa mbele za BWANA wakilia. Wakafunga siku ile mpaka jioni na kutoa sadaka ya kutekezwa na sadaka ya amani kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Waisraeli, watu wote, wakapanda Betheli, huko wakakaa mbele za bwana wakilia. Wakafunga siku ile mpaka jioni na kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo wana wa Israeli wote, na hao watu wote, wakakwea, wakaenda Betheli, na kulia, wakaketi hapo mbele za BWANA, wakafunga siku hiyo hadi jioni; nao wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote wa jeshi la Waisraeli wakaenda Betheli. Walikaa huko mbele ya Mwenyezi-Mungu wakiomboleza na kufunga mpaka jioni. Wakamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wana wote wa Isiraeli nao watu wote walipopanda kwenda Beteli, wakamlilia Bwana huko pasipo kukoma, wakafunga siku hiyo mchana kutwa wakimtolea Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za shukrani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo wana Israeli wote, na hao watu wote, wakakwea, wakaenda Betheli, na kulia, wakaketi hapo mbele za BWANA, wakafunga siku hiyo hata jioni; nao wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote wa jeshi la Waisraeli wakaenda Beteli. Wakaikaa kule mbele ya Yawe wakiomboleza na kufunga mpaka magaribi. Wakamutolea Yawe sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani.