Judges 20:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha watu wa kabila la Benyamini walipotoka mjini kuanza kupigana na Waisraeli, walivutwa kutoka nje ya mji. Ilitokea tena kama walivyofanya nyakati za hapo awali wakawaua baadhi ya watu wa Israeli kwenye njia kuu zielekeazo miji ya Betheli na Gibea, mpaka mbugani. Waliua Waisraeli wapatao thelathini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wabenyamini wakatoka ili kukabiliana na Waisraeli, ambao waliwavuta Wabenyamini watoke katika mji. Wakaanza kupigana na wakawaua watu wapatao thelathini wa Israeli, kama walivyofanya nyakati nyingine, katika uwanja na katika njia kuu, moja iendayo Betheli na nyingine Gibea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wana wa Benyamini wakatoka waende kupigana nao, wakavutwa waende mbali na huo mji; kisha wakaanza kupiga na kuua katika hao watu, wapata kama watu thelathini wa Israeli, kama walivyofanya nyakati nyingine, katika hizo njia kuu, ambazo njia mojawapo huendelea Betheli, na njia ya pili huendelea Gibea, katika shamba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha watu wa kabila la Benyamini walipotoka mjini kuanza kupigana na Waisraeli, walivutwa kutoka nje ya mji. Ilitokea tena kama walivyofanya nyakati za hapo awali wakawaua baadhi ya watu wa Israeli kwenye njia kuu zielekeazo miji ya Betheli na Gibea, mpaka mbugani. Waliua Waisraeli wapatao thelathini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wabenyamini wakatoka ili kukabiliana nao, Waisraeli wakawavuta Wabenyamini watoke katika mji. Wakaanza kupigana na kuua watu wapatao thelathini wa Israeli, kama walivyofanya nyakati nyingine, katika njia kuu, moja iendayo Betheli na nyingine Gibea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wabenyamini wakatoka ili kukabiliana nao, Waisraeli wakawavuta Wabenyamini watoke katika mji. Wakaanza kupigana na kuua watu wapatao thelathini wa Israeli, kama walivyofanya nyakati nyingine, katika njia kuu, moja iendayo Betheli na nyingine Gibea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wana wa Benyamini wakatoka waende kupigana nao, wakavutwa waende mbali na huo mji; kisha wakaanza kuwapiga na kuwaua Waisraeli wapatao thelathini, kama walivyofanya hapo awali, kwa kuwaua katika hizo njia kuu, zielekeazo Betheli, na Gibea, na katika nchi tambarare.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha watu wa kabila la Benyamini walipotoka mjini kuanza kupigana na Waisraeli, walivutwa kutoka nje ya mji. Ilitokea tena kama walivyofanya nyakati za hapo awali wakawaua baadhi ya watu wa Israeli kwenye njia kuu zielekeazo miji ya Betheli na Gibea, mpaka mbugani. Waliua Waisraeli wapatao thelathini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Benyamini nao wakatoka kukutana nao, wakatengekana na mji wa kwao; walipoanza kupiga watu wengine kama jana na juzi na kuwaumiza hapo barabarani watu wa Waisiraeli 30, palikuwa hapo, barabara moja inapokwenda kupanda Beteli, ya pili inakwenda Gibea na kupita mashambani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wana wa Benyamini wakatoka waende kupigana nao, wakavutwa waende mbali na huo mji; kisha wakaanza kupiga na kuua katika hao watu, wapata kama watu thelathini wa Israeli, kama walivyofanya nyakati nyingine, katika hizo njia kuu, ambazo njia mojawapo huendelea Betheli, na njia ya pili huendelea Gibea, katika shamba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha watu wa kabila la Benjamina walipotoka katika muji kwa kuanza kupigana na Waisraeli, walivutwa kutoka inje ya muji. Ilitokea tena kama walivyofanya nyakati za mbele. Wakawaua wamoja kati ya watu wa Israeli kwenye njia kubwa zinazoelekea miji ya Beteli na Gibea, mpaka katika mbuga. Waliua Waisraeli yapata makumi tatu.