Judges 20:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Askari hodari waliochaguliwa kutoka makabila yote ya Israeli wakawasili hapo mbele ya mji wa Gibea. Vita vya siku hiyo vilikuwa vikali. Lakini watu wa Benyamini hawakufahamu kwamba kuangamia kwao kulikuwa karibu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo vijana wenye uwezo elfu kumi katika Israeli wakaja kuishambulia Gibea. Vita vilikuwa vikali sana, hata Wabenyamini hawakutambua kuwa maangamizi yalikuwa karibu nao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha watu elfu kumi waliochaguliwa katika Israeli wote wakaja juu ya Gibea, na vile vita vilikuwa vikali sana; lakini hawakujua ya kuwa uovu ulikuwa karibu nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Askari hodari waliochaguliwa kutoka makabila yote ya Israeli wakawasili hapo mbele ya mji wa Gibea. Vita vya siku hiyo vilikuwa vikali. Lakini watu wa Benyamini hawakufahamu kwamba kuangamia kwao kulikuwa karibu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo watu 10,000 bora waliochaguliwa katika Israeli wote, wakaja kuishambulia Gibea. Vita vilikuwa vikali sana, hata Wabenyamini hawakutambua kuwa maangamizi yalikuwa karibu nao kwa kiasi hicho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo watu 10,000 bora waliochaguliwa katika Israeli wote, wakaja kuishambulia Gibea. Vita vilikuwa vikali sana, hata Wabenyamini hawakutambua kuwa maangamizi yalikuwa karibu nao kwa kiasi hicho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha watu elfu kumi waliochaguliwa katika Israeli wote wakavamia Gibea, na vile vita vilikuwa vikali sana; lakini Benyamini hawakujua ya kuwa maafa yalikuwa karibu nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Askari hodari waliochaguliwa kutoka makabila yote ya Israeli wakawasili hapo mbele ya mji wa Gibea. Vita vya siku hiyo vilikuwa vikali. Lakini watu wa Benyamini hawakufahamu kwamba kuangamia kwao kulikuwa karibu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, watu 10000 waliochaguliwa katika Waisiraeli wote walivyoujia Gibea toka ng'ambo ya huko; ndipo, mapigano yalipokuwa makali, nao walikuwa hawajajua bado, ya kuwa mambo mabaya yamewapata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha watu elfu kumi waliochaguliwa katika Israeli wote wakaja juu ya Gibea, na vile vita vilikuwa vikali sana; lakini hawakujua ya kuwa uovu ulikuwa karibu nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waaskari hodari waliochaguliwa kutoka makabila yote ya Israeli wakafika pale mbele ya muji wa Gibea. Vita ya siku hiyo ilikuwa kali. Lakini watu wa Benjamina hawakufahamu kwamba kuangamia kwao kulikuwa karibu.