Judges 20:35 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu aliwashinda watu wa Benyamini mbele ya Waisraeli. Waisraeli wakawaua watu wa Benyamini 25,100. Hao wote waliouawa walikuwa askari walioweza kutumia silaha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akawashinda Wabenyamini mbele ya Waisraeli, na siku hiyo Waisraeli wakawaua Wabenyamini elfu ishirini na tano na mia moja wenye panga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akampiga Benyamini mbele ya Israeli; na wana wa Israeli waliangamiza watu waume ishirini na tano elfu na mia moja, wa Benyamini siku hiyo; wote hao waliokuwa wenye kutumia upanga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu aliwashinda watu wa Benyamini mbele ya Waisraeli. Waisraeli wakawaua watu wa Benyamini 25,100. Hao wote waliouawa walikuwa askari walioweza kutumia silaha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akawashinda Wabenyamini mbele ya Waisraeli na siku ile Waisraeli wakawaua Wabenyamini watu waume 25,100, wote wakiwa wenye kujifunga silaha za vita.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akawashinda Wabenyamini mbele ya Waisraeli na siku ile Waisraeli wakawaua Wabenyamini watu waume 25,100, wote wakiwa wenye kujifunga silaha za vita.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akampiga Benyamini mbele ya Israeli; na wana wa Israeli waliangamiza wanaume elfu ishirini na tano na mia moja, wa Benyamini siku hiyo; wote hao waliokuwa wenye kutumia upanga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu aliwashinda watu wa Benyamini mbele ya Waisraeli. Waisraeli wakawaua watu wa Benyamini 25,100. Hao wote waliouawa walikuwa askari walioweza kutumia silaha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, Bwana alivyowapiga Wabenyamini mbele ya Waisiraeli, nao wana wa Isiraeli wakawafanyizia Wabenyamini mabaya siku hiyo kwa kuangamiza watu 25100, nao hao wote walijua kuchomoa panga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akampiga Benyamini mbele ya Israeli; na wana wa Israeli waliangamiza watu waume ishirini na tano elfu na mia moja, wa Benyamini siku hiyo; wote hao waliokuwa wenye kutumia upanga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akawashinda watu wa Benjamina mbele ya Waisraeli. Waisraeli wakawaua watu wa Benjamina elfu makumi mbili na tano na mia moja. Hao wote waliouawa walikuwa waaskari walioweza kutumia silaha.