Judges 20:36 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo watu wa kabila la Benyamini wakaona kwamba wameshindwa. Waisraeli walirudi nyuma kana kwamba wanawakimbia watu wa kabila la Benyamini, kwani walitegemea wenzao waliokuwa wamewekwa kuotea mji wa Gibea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Wabenyamini wakaona kuwa wameshindwa. Basi Waisraeli walikuwa wamewaondokea Wabenyamini, kwa sababu Waisraeli waliwategemea hao waviziaji waliokuwa wamewaweka karibu na Gibea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wana wa Benyamini waliona kuwa wamepigwa; kwa kuwa watu wa Israeli wakaondoka mbele ya Benyamini, kwa sababu walikuwa wanawatumaini hao wenye kuvizia waliokuwa wamewaweka kinyume cha Gibea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo watu wa kabila la Benyamini wakaona kwamba wameshindwa. Waisraeli walirudi nyuma kana kwamba wanawakimbia watu wa kabila la Benyamini, kwani walitegemea wenzao waliokuwa wamewekwa kuotea mji wa Gibea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Wabenyamini wakaona kuwa wamepigwa. Basi Waisraeli walikuwa wameondoka mbele ya Wabenyamini, kwa sababu Waisraeli waliwategemea hao waviziaji waliokuwa wamewaweka dhidi ya Gibea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Wabenyamini wakaona kuwa wamepigwa. Basi Waisraeli walikuwa wameondoka mbele ya Wabenyamini, kwa sababu Waisraeli waliwategemea hao waviziaji waliokuwa wamewaweka dhidi ya Gibea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wana wa Benyamini waliona kuwa wamepigwa. Watu wa Israeli wakaondoka mbele ya Benyamini, kwa sababu walikuwa wanawatumaini hao wenye kuvizia waliokuwa wamewaweka kinyume cha Gibea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo watu wa kabila la Benyamini wakaona kwamba wameshindwa. Waisraeli walirudi nyuma kana kwamba wanawakimbia watu wa kabila la Benyamini, kwani walitegemea wenzao waliokuwa wamewekwa kuotea mji wa Gibea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wana wa Benyamini walipoona, ya kuwa wamekwisha kupigwa. Lakini Waisiraeli waliendelea kuwaachia Wabenyamini mahali pao, walipokuwa, kwani waliwaegemea wao waviziao, waliowaweka ng'ambo ya huko ya Gibea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wana wa Benyamini waliona kuwa wamepigwa; kwa kuwa watu wa Israeli wakaondoka mbele ya Benyamini, kwa sababu walikuwa wanawatumaini hao wenye kuvizia waliokuwa wamewaweka kinyume cha Gibea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo watu wa kabila la Benjamina wakaona kwamba wameshindwa. Waisraeli wakarudi nyuma sawa vile wanawakimbia watu wa kabila la Benjamina, maana walitegemea wenzao waliokuwa wamewekwa kufichamia muji wa Gibea.