Judges 20:40 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini ile ishara ya mnara wa moshi ilipoanza kutokea katika mji, watu wa kabila la Benyamini walipotazama nyuma yao, wakashangaa kuona kwamba mji wao ulikuwa unateketezwa moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini nguzo ya moshi ilipoanza kupanda kutoka mji ule, Wabenyamini wakageuka, na tazama: katika mji mzima, moshi ulikuwa ukipaa angani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini hapo hilo wingu lilipoanza kupanda kutoka katika mji, kama nguzo ya moshi, ndipo Wabenyamini wakaangalia nyuma, na tazama, huo mji mzima ulikuwa wapaa juu katika moshi kwenda mbinguni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini ile ishara ya mnara wa moshi ilipoanza kutokea katika mji, watu wa kabila la Benyamini walipotazama nyuma yao, wakashangaa kuona kwamba mji wao ulikuwa unateketezwa moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wakati lile wingu la moshi lilipoanza kupanda kutoka katika ule mji, Wabenyamini wakageuka na kuona moshi wa mji mzima unapaa juu angani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wakati lile wingu la moshi lilipoanza kupanda kutoka ule mji, Wabenyamini wakageuka na kuona moshi wa mji mzima unapaa juu angani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini hapo hilo wingu lilipoanza kupanda kutoka katika mji, kama nguzo ya moshi, ndipo Wabenyamini wakaangalia nyuma, na tazama, moshi ulikuwa umetanda mji mzima kwenda mbinguni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini ile ishara ya mnara wa moshi ilipoanza kutokea katika mji, watu wa kabila la Benyamini walipotazama nyuma yao, wakashangaa kuona kwamba mji wao ulikuwa unateketezwa moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara kile kielekezo cha moto kikaanza kupanda juu, lile wingu la moshi; nao Wabenyamini walipogeuka nyuma yao, wakaona, mji wote mzima ulivyoteketea na kupandisha moshi mbinguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini hapo hilo wingu lilipoanza kupanda kutoka katika mji, kama nguzo ya moshi, ndipo Wabenyamini wakaangalia nyuma, na tazama, huo mji mzima ulikuwa wapaa juu katika moshi kwenda mbinguni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kile kitambulisho cha moshi kilipoanza kutokea katika muji, watu wa kabila la Benjamina wakaangalia nyuma yao, wakashangaa kuona kwamba muji wao ulikuwa unateketezwa kwa moto.