Judges 20:45 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wengine wa kabila la Benyamini waligeuka, wakakimbia kuelekea jangwani hadi mwamba wa Rimoni. Wengine 5,000 waliuawa kwenye njia kuu walipokuwa wanakimbia. Waisraeli waliendelea kuwafuatia vikali watu wa kabila la Benyamini hadi mji wa Gidomu wakawaua watu 2,000.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipogeuka na kukimbia kuelekea nyikani hata kufikia mwamba wa Rimoni, Waisraeli wakawaua watu elfu tano huko njiani. Wakawafuatia kwa karibu hadi Gidomu, na huko wakawaua wanaume wengine elfu mbili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wakageuka na kukimbia upande wa nyika hata kulifikilia jabali la Rimoni; nao wakaokota katika watu hao katika njia kuu watu waume elfu tano; wakawaandamia kwa kasi mpaka Gidomu, nako wakawapiga wengine wao watu elfu mbili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wengine wa kabila la Benyamini waligeuka, wakakimbia kuelekea jangwani hadi mwamba wa Rimoni. Wengine 5,000 waliuawa kwenye njia kuu walipokuwa wanakimbia. Waisraeli waliendelea kuwafuatia vikali watu wa kabila la Benyamini hadi mji wa Gidomu wakawaua watu 2,000.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipogeuka na kukimbia kuelekea nyikani hata kufikia mwamba wa Rimoni, Waisraeli wakawaua watu 5,000 wakiwa njiani. Wakawafuatia kwa kasi mpaka Gidomu huko wakawaua watu wengine 2,000.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipogeuka na kukimbia kuelekea nyikani hata kufikia mwamba wa Rimoni, Waisraeli wakawaua watu 5,000 wakiwa njiani. Wakawafuata kwa kasi mpaka Gidomu huko wakawaua watu wengine 2,000.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wakageuka na kukimbilia upande wa nyika hadi katika jabali la Rimoni; nao wakaokota katika watu hao katika njia kuu wanaume elfu tano; wakawaandamia kwa kasi mpaka Gidomu, nako wakawaua wengine wao watu elfu mbili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wengine wa kabila la Benyamini waligeuka, wakakimbia kuelekea jangwani hadi mwamba wa Rimoni. Wengine 5,000 waliuawa kwenye njia kuu walipokuwa wanakimbia. Waisraeli waliendelea kuwafuatia vikali watu wa kabila la Benyamini hadi mji wa Gidomu wakawaua watu 2,000.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipogeuka kukimbilia nyikani kwenye mwamba wa Rimoni; lakini wale wakawaokoteza barabarani na kuua tena 5000, wakagandamana nao kwa kuwafuata hata Gidomu, huko nako wakaua wengine wao 2000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wakageuka na kukimbia upande wa nyika hata kulifikilia jabali la Rimoni; nao wakaokota katika watu hao katika njia kuu watu waume elfu tano; wakawaandamia kwa kasi mpaka Gidomu, nako wakawapiga wengine wao watu elfu mbili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wengine wa kabila la Benjamina wakakimbia kuelekea upande wa jangwa mpaka kwenye mulima wa Rimoni. Wengine elfu tano waliuawa kwenye njia kubwa walipokuwa wanakimbia. Waisraeli waliendelea kuwafuatilia vikali watu wa kabila la Benjamina mpaka kwenye muji wa Gidomu, wakawaua watu elfu mbili.