Judges 20:48 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli wakawageukia watu wengine wa kabila la Benyamini, wakawaua wote: Wanaume, wanawake, watoto na wanyama. Na miji yote waliyoikuta huko wakaiteketeza moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli wakarudi na kuwaua kwa upanga Wabenyamini wote, pamoja na wanyama na kila walichokipata. Pia kila mji waliouona wakauchoma kwa moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha watu wa Israeli wakageuka tena kuwaendea wana wa Benyamini, wakawapiga kwa makali ya upanga, huo mji mzima, na hao wanyama wa mji, na kila kitu walichokiona; tena miji yote waliyoiona wakaitia moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli wakawageukia watu wengine wa kabila la Benyamini, wakawaua wote: wanaume, wanawake, watoto na wanyama. Na miji yote waliyoikuta huko wakaiteketeza moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli wakarudi na kuua watu wote wa Benyamini, pamoja na wanyama na kila walichokikuta. Pia kila mji waliouona waliuchoma moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli wakarudi na kuua watu wote wa Benyamini, pamoja na wanyama na kila walichokikuta. Pia kila mji waliouona waliuchoma moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha watu wa Israeli wakageuka tena kuwaendea wana wa Benyamini, wakawapiga kwa makali ya upanga, huo mji mzima, na hao wanyama wa mji, na kila kitu walichokiona; tena miji yote waliyoiona wakaiteketeza kwa moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli wakawageukia watu wengine wa kabila la Benyamini, wakawaua wote: Wanaume, wanawake, watoto na wanyama. Na miji yote waliyoikuta huko wakaiteketeza moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Waisiraeli wakawarudia wana wa Benyamini, wakawapiga kwa ukali wa panga wote walioonekana, watu wa mijini pia hata nyama; nayo miji yote iliyopatikana wakaiteketeza kwa moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha watu wa Israeli wakageuka tena kuwaendea wana wa Benyamini, wakawapiga kwa makali ya upanga, huo mji mzima, na hao wanyama wa mji, na kila kitu walichokiona; tena miji yote waliyoiona wakaitia moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli wakawageukia watu wengine wa kabila la Benjamina, wakawaua wote: wanaume, wanawake, watoto na nyama. Na miji yote waliyoikuta kule wakaiteketeza kwa moto.