Judges 20:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini watu wa mji wa Gibea wakaja usiku wakaizingira nyumba nilimokuwa nimelala. Walitaka kuniua, wakambaka suria wangu mpaka akafa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wa usiku wanaume wa Gibea wakanijia na kuizingira nyumba, wakitaka kuniua. Wakambaka suria wangu hata akafa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watu waume wa Gibea wakaniondokea, na kuizingira hiyo nyumba pande zote juu yangu wakati wa usiku; walidhani kuniua, na suria wangu wakamtenza nguvu, hata amekufa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini watu wa mji wa Gibea wakaja usiku wakaizingira nyumba nilimokuwa nimelala. Walitaka kuniua, wakambaka suria wangu mpaka akafa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa usiku watu wa Gibea wakanijia na kuizingira nyumba, wakitaka kuniua. Wakambaka suria wangu mpaka akafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa usiku watu wa Gibea wakanijia na kuizingira nyumba, wakitaka kuniua. Wakambaka suria wangu mpaka akafa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wanaume wa Gibea wakaniondokea, na kuizingira hiyo nyumba pande zote juu yangu wakati wa usiku; walitaka kuniua, na suria wangu wakambaka nguvu, hata akafa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini watu wa mji wa Gibea wakaja usiku wakaizingira nyumba nilimokuwa nimelala. Walitaka kuniua, wakambaka suria wangu mpaka akafa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wenyeji wa Gibea wakaniinukia; ulipokuwa usiku, wakaizunguka hiyo nyumba, nilimokuwa, wakataka kuniua mimi, naye suria yangu wakamkorofisha, mpaka akifa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watu waume wa Gibea wakaniondokea, na kuizingira hiyo nyumba pande zote juu yangu wakati wa usiku; walidhani kuniua, na suria wangu wakamtenza nguvu, hata amekufa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini watu wa muji wa Gibea wakakuja usiku wakaizunguka nyumba nilimokuwa nimelala. Wakataka kuniua, wakamutendea kwa kinguvu habara yangu mpaka akakufa.