Judges 21:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi wakakuta miongoni mwa wakazi wa Yabesh-gileadi wasichana 400 ambao hawakuwa wamelala na mwanamume yeyote, wakawapeleka kambini huko Shilo katika nchi ya Kanaani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakapata kati ya watu walioishi Yabesh-Gileadi wanawali mia nne, mabikira, nao wakawachukua kwenye kambi huko Shilo katika nchi ya Kanaani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakapata katika wenyeji wa Yabesh-gileadi wanawali mia nne, ambao hawajamjua mtu mume kwa kulala naye; basi wakawaleta maragoni huko Shilo, ulioko katika nchi ya Kanaani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi wakakuta miongoni mwa wakazi wa Yabesh-gileadi wasichana 400 ambao hawakuwa wamelala na mwanamume yeyote, wakawapeleka kambini huko Shilo katika nchi ya Kanaani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakawakuta watu waishio Yabeshi-Gileadi wanawali mia nne ambao hawajakutana kimwili, nao wakawachukuwa kwenye kambi huko Shilo katika nchi ya Kanaani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakakuta kati ya watu walioishi Yabeshi-Gileadi wanawali mia nne ambao hawajakutana kimwili na mwanaume, nao wakawachukua kwenye kambi huko Shilo katika nchi ya Kanaani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakapata katika wenyeji wa Yabesh-gileadi wanawali mia nne, ambao hawajamjua mwanamume kwa kulala naye; basi wakawaleta kambini huko Shilo, ulioko katika nchi ya Kanaani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi wakakuta miongoni mwa wakazi wa Yabesh-gileadi wasichana 400 ambao hawakuwa wamelala na mwanamume yeyote, wakawapeleka kambini huko Shilo katika nchi ya Kanaani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwao wenyeji wa Yabesi wa Gileadi wakaonekana wanawali 400 wasiotambua bado mtu mume kwa kulala naye; hao wakawapeleka katika makambi ya Silo ulioko katika nchi ya Kanaani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakapata katika wenyeji wa Yabesh-gileadi wanawali mia nne, ambao hawajamjua mtu mume kwa kulala naye; basi wakawaleta maragoni huko Shilo, ulioko katika nchi ya Kanaani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wakakuta kati ya wakaaji wa Yabesi-Gileadi wabinti mia ine ambao hawakukuwa wamekwisha kulala na mwanaume yeyote, wakawapeleka katika kambi kule Shilo katika inchi ya Kanana.