Judges 21:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli wakawaonea huruma watu wa kabila la Benyamini, maana Mwenyezi-Mungu alisababisha kuweko na mwanya katika Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli wakahuzunika kwa ajili ya Wabenyamini, kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa ameweka ufa katika makabila ya Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watu wakaghairi kwa ajili ya Benyamini, kwa sababu Bwana alikuwa amefanya pengo katika hizo kabila za Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli wakawaonea huruma watu wa kabila la Benyamini, maana Mwenyezi-Mungu alisababisha kuweko na mwanya katika Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli wakasikitika kwa ajili ya Wabenyamini, kwa kuwa BWANA ameweka ufa katika makabila ya Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli wakasikitika kwa ajili ya Wabenyamini, kwa kuwa bwana ameweka ufa katika makabila ya Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watu wakawahurumia Wabenyamini, kwa sababu BWANA alikuwa amefanya pengo katika hayo makabila ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli wakawaonea huruma watu wa kabila la Benyamini, maana Mwenyezi-Mungu alisababisha kuweko na mwanya katika Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watu wakawaonea Wabenyamini uchungu, kwa kuwa Bwana amewatenga Waisiraeli, patokee ufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watu wakaghairi kwa ajili ya Benyamini, kwa sababu BWANA alikuwa amefanya pengo katika hizo kabila za Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli wakawaonea huruma watu wa kabila la Benjamina, maana Yawe alisababisha kukuwe shimo kati ya Waisraeli.