Judges 21:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi wakakumbuka kwamba sikukuu ya Mwenyezi-Mungu iliyofanyika kila mwaka huko Shilo, mji ulio kaskazini ya Betheli, kwenye njia kuu itokayo Betheli kwenda Shekemu, ilikuwa inakaribia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo waliposema, “Tazama iko sikukuu ya kila mwaka ya Mwenyezi Mungu katika Shilo, kaskazini mwa Betheli na mashariki mwa ile barabara inayotoka Betheli kwenda Shekemu, upande wa kusini wa Lebona.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wakasema, Angalieni, iko sikukuu ya Bwana mwaka baada ya mwaka katika Shilo, ulioko upande kaskazini wa Betheli, upande wa mashariki wa hiyo njia kuu iendeayo kutoka Betheli kwenda Shekemu, nao ni upande wa kusini wa Lebona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi wakakumbuka kwamba sikukuu ya Mwenyezi-Mungu iliyofanyika kila mwaka huko Shilo, mji ulio kaskazini ya Betheli, kwenye njia kuu itokayo Betheli kwenda Shekemu, ilikuwa inakaribia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo waliposema, “Tazama iko sikukuu ya kila mwaka ya BWANA katika Shilo, kaskazini ya Betheli na mashariki mwa ile barabara itokayo Betheli kwenda Shekemu, nako ni kusini ya Lebona.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo waliposema, “Tazama iko sikukuu ya kila mwaka ya bwana katika Shilo, kaskazini ya Betheli na mashariki mwa ile barabara itokayo Betheli kwenda Shekemu, upande wa kusini wa Lebona.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wakasema, Angalieni, iko sikukuu ya BWANA mwaka baada ya mwaka katika Shilo, mji ulio upande wa kaskazini mwa Betheli, upande wa mashariki mwa hiyo njia kuu iendeayo kutoka Betheli kwenda Shekemu, nao ni upande wa kusini mwa Lebona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi wakakumbuka kwamba sikukuu ya Mwenyezi-Mungu iliyofanyika kila mwaka huko Shilo, mji ulio kaskazini ya Betheli, kwenye njia kuu itokayo Betheli kwenda Shekemu, ilikuwa inakaribia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakasema: Tazameni! Mwaka kwa mwaka iko sikukuu ya Bwana huko Silo ulioko karibu ya Beteli upande wa kaskazini, ni hapo penye barabara itokayo Beteli kwenda Sikemu upande wa maawioni kwa jua, tena ni karibu ya Lebona upande wa kusini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wakasema, Angalieni, iko sikukuu ya BWANA mwaka baada ya mwaka katika Shilo, ulioko upande kaskazini wa Betheli, upande wa mashariki wa hiyo njia kuu iendeayo kutoka Betheli kwenda Shekemu, nao ni upande wa kusini wa Lebona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wakakumbuka kwamba sikukuu ya Yawe iliyofanyika kila mwaka kule Shilo, muji unaokuwa upande wa kaskazini wa Beteli, kwenye njia kubwa inayotoka Beteli kwenda Sekemu, ilikuwa inakaribia.