Judges 21:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baba zao au kaka zao wakija kutulalamikia tutawaambia, “Sisi tunawaombeni mwahurumie watu wa Benyamini na kuwaachia wawachukue hao wanawake; maana hatukuwapata katika vita vya Yabesh-gileadi. Na kwa vile nyinyi wenyewe hamkutupatia hao binti zenu, hamtahukumiwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baba zao au ndugu zao watakapotulalamikia, tutawaambia, ‘Kuweni wakarimu kwetu, nanyi mturuhusu tuwe nao kwa kuwa hatukuweza kumpa kila mtu mke tulipopigana. Lakini ninyi pia hamna hatia, kwa kuwa hamkuwapa wao binti zenu kuwa wake.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha itakuwa, hapo baba zao au ndugu zao, watakapokuja kushitaki, sisi tutawaambia, Kwa ihisani yenu tupeni sisi; kwa kuwa hatukumtwalia kila mtu mkewe katika vita; wala ninyi hamkuwapa wao, au kama sivyo ninyi sasa mngekuwa na hatia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baba zao au kaka zao wakija kutulalamikia tutawaambia, “Sisi tunawaombeni mwahurumie watu wa Benyamini na kuwaachia wawachukue hao wanawake; maana hatukuwapata katika vita vya Yabesh-gileadi. Na kwa vile nyinyi wenyewe hamkutupatia hao binti zenu, hamtahukumiwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baba zao au ndugu zao waume watakapotulalamikia, tutawaambia, ‘Iweni wakarimu kwetu, nanyi mturuhusu tuwe nao kwa kuwa hatukuweza kumpatia kila mtu mke tulipopigana. Lakini ninyi pia hamna hatia kwa kuwapa wao binti zenu kuwa wake.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baba zao au ndugu zao waume watakapotulalamikia, tutawaambia, ‘Kuweni wakarimu kwetu, nanyi mturuhusu tuwe nao kwa kuwa hatukuweza kumpa kila mtu mke tulipopigana. Lakini ninyi pia hamna hatia kwa kuwa hamkuwapa wao binti zenu kuwa wake.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha baba zao au ndugu zao watakapokuja kushitaki, sisi tutawaambia, Kwa hisani yenu tupeni sisi; kwa kuwa hatukumtwalia kila mtu mkewe katika vita; na kwa kuwa hamkuwapa wao, la sivyo ninyi sasa mngekuwa na hatia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baba zao au kaka zao wakija kutulalamikia tutawaambia, “Sisi tunawaombeni mwahurumie watu wa Benyamini na kuwaachia wawachukue hao wanawake; maana hatukuwapata katika vita vya Yabesh-gileadi. Na kwa vile nyinyi wenyewe hamkutupatia hao binti zenu, hamtahukumiwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama baba zao au ndugu zao watakuja kutugombeza, tutawaambia: Waacheni kuwa matunzo, mnayotupa sisi, kwa kuwa vitani hatukumpatia kila mtu mkewe. Hivyo ninyi hamtawatoa kuwapa wale; kama mngewapa wenyewe, mngekora manza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha itakuwa, hapo baba zao au ndugu zao, watakapokuja kushitaki, sisi tutawaambia, Kwa ihisani yenu tupeni sisi; kwa kuwa hatukumtwalia kila mtu mkewe katika vita; wala ninyi hamkuwapa wao, au kama sivyo ninyi sasa mngekuwa na hatia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Baba zao au kaka zao wakikuja kutulalamikia tutawaambia: “Sisi tunawaomba muwahurumie watu wa Benjamina na kuwaacha watwae hao wanawake; maana hatukupata wanawake wa kutosha katika vita ya Yabesi-Gileadi. Na kwa sababu si ninyi wenyewe muliowapatia hao wabinti zenu, hamutahukumiwa kwamba mumevunja kiapo.”