Judges 21:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale wanaume wa kabila la Benyamini wakafanya hivyo, kila mmoja akajichagulia msichana miongoni mwa wasichana waliotoka nje kucheza huko Shilo na kumchukua kuwa mkewe. Kisha wakarudi katika eneo lao, wakaijenga miji yao upya na kuishi humo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi hivyo ndivyo Wabenyamini walivyofanya. Wasichana walipokuwa wakicheza, kila mtu akanyakua msichana mmoja, akaenda naye ili awe mke wake. Kisha wakarudi katika urithi wao na kuijenga upya miji na kuishi humo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wa Benyamini wakafanya vivyo, wakajitwalia wake, sawasawa na hesabu yao, katika hao waliocheza, wakawachukua wakaenda nao; kisha wakaenda kuurudia urithi wao, na kuijenga miji na kuikaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale wanaume wa kabila la Benyamini wakafanya hivyo, kila mmoja akajichagulia msichana miongoni mwa wasichana waliotoka nje kucheza huko Shilo na kumchukua kuwa mkewe. Kisha wakarudi katika eneo lao, wakaijenga miji yao upya na kuishi humo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi hivyo ndivyo Wabenyamini walivyofanya. Wakati wasichana walipokuwa wakicheza, kila mtu akamkamata msichana mmoja akamchukua akaenda naye ili awe mke wake. Kisha wakarudi katika urithi wao na kuijenga upya miji na kuishi humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi hivyo ndivyo Wabenyamini walivyofanya. Wakati wasichana walipokuwa wakicheza, kila mtu akamkamata msichana mmoja akamchukua akaenda naye ili awe mke wake. Kisha wakarudi katika urithi wao na kuijenga upya miji na kuishi humo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wana wa Benyamini wakafanya hivyo, wakajitwalia wake, kulingana na hesabu yao, katika hao waliocheza, wakawachukua wakaenda nao; kisha wakaenda kuurudia urithi wao, na kuijenga miji na kuishi humo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale wanaume wa kabila la Benyamini wakafanya hivyo, kila mmoja akajichagulia msichana miongoni mwa wasichana waliotoka nje kucheza huko Shilo na kumchukua kuwa mkewe. Kisha wakarudi katika eneo lao, wakaijenga miji yao upya na kuishi humo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Benyamini wakavifanya hivyo, wakachukua wanawake na kuwanyang'anya kwa hesabu yao kwao waliocheza michezo yao, kisha wakaenda zao, wakarudi katika nchi iliyokuwa fungu lao, wakajenga miji, wakakaa humo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wa Benyamini wakafanya vivyo, wakajitwalia wake, sawasawa na hesabu yao, katika hao waliocheza, wakawachukua wakaenda nao; kisha wakaenda kuurudia urithi wao, na kuijenga miji na kuikaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wanaume wa kabila la Benjamina wakafanya hivyo, kila mumoja akajichagulia binti kati ya wabinti waliotoka inje kwa kucheza kule Shilo na kumutwaa kuwa muke wake. Kisha wakarudi katika eneo lao, wakaijenga miji yao upya na kuishi mule.