Judges 21:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha wakaulizana, “Je, miongoni mwa makabila yote ya Israeli kuna kikundi chochote ambacho hakikuhudhuria mkutano uliofanyika mbele ya Mwenyezi-Mungu?” Walikuwa wamefanya kiapo kwamba mtu yeyote ambaye hatahudhuria mbele ya Mwenyezi-Mungu huko Mizpa ni lazima auawe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Waisraeli wakauliza, “Ni kabila lipi la Israeli ambalo halikukusanyika mbele za Mwenyezi Mungu?” Kwa kuwa walikuwa wameapa kiapo kikuu kuwa yeyote asiyefika mbele za Mwenyezi Mungu huko Mispa, kwa hakika angeuawa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wa Israeli wakasema, Katika hizi kabila zote za Israeli ni ipi isiyofika katika mkutano kumkaribia Bwana? Kwa maana walikuwa wameweka kiapo kikuu katika habari za huyo asiyefika kumkaribia Bwana huko Mispa, huku wakisema, Hakika yake atauawa huyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha wakaulizana, “Je, miongoni mwa makabila yote ya Israeli kuna kikundi chochote ambacho hakikuhudhuria mkutano uliofanyika mbele ya Mwenyezi-Mungu?” Walikuwa wamefanya kiapo kwamba mtu yeyote ambaye hatahudhuria mbele ya Mwenyezi-Mungu huko Mizpa ni lazima auawe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Waisraeli wakasema, “Ni kabila lipi la Israeli ambalo halikufika katika mkutano kumkaribia BWANA?” Kwa kuwa walikuwa wameweka kiapo kikuu kuwa ye yote asiyefika mbele za BWANA huko Mispa, kwa hakika angeuawa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Waisraeli wakasema, “Ni kabila lipi la Israeli ambalo halikufika katika mkutano kumkaribia bwana?” Kwa kuwa walikuwa wameweka kiapo kikuu kuwa yeyote asiyefika mbele za bwana huko Mispa, kwa hakika angeuawa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wana wa Israeli wakasema, Katika hizi kabila zote za Israeli ni ipi isiyofika katika mkutano kumkaribia BWANA? Kwa maana walikuwa wameweka kiapo kikuu kuhusu huyo asiyefika kumkaribia BWANA huko Mispa, huku wakisema, Hakika yake atauawa huyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha wakaulizana, “Je, miongoni mwa makabila yote ya Israeli kuna kikundi chochote ambacho hakikuhudhuria mkutano uliofanyika mbele ya Mwenyezi-Mungu?” Walikuwa wamefanya kiapo kwamba mtu yeyote ambaye hatahudhuria mbele ya Mwenyezi-Mungu huko Mizpa ni lazima auawe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wana wa Isiraeli walipoulizana: Je? Katika mashina yote ya Waisiraeli wako wasiopanda kumtokea Bwana penye mkutano huu hapa Misipa? Kwani walikuwa wameapiana kiapo kikuu cha kwamba: Wao watakaokaa, wasipande kumtokea Bwana, hawana budi kuuawa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wa Israeli wakasema, Katika hizi kabila zote za Israeli ni ipi isiyofika katika mkutano kumkaribia BWANA? Kwa maana walikuwa wameweka kiapo kikuu katika habari za huyo asiyefika kumkaribia BWANA huko Mispa, huku wakisema, Hakika yake atauawa huyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha wakaulizana: “Kati ya makabila yote ya Israeli kuna kikundi chochote ambacho hakikuhuzuria mukutano uliofanyika mbele ya Yawe?” Walikuwa wamefanya kiapo kwamba mutu yeyote ambaye hatahuzuria mbele ya Yawe kule Misipa anapaswa kuuawa.