Judges 3:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Othnieli, naye akawa mwamuzi wa Waisraeli. Othnieli alikwenda vitani naye Mwenyezi-Mungu akamtia Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia mikononi mwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu yake; hivyo akawa mwamuzi wa Israeli, na akaenda vitani. Mwenyezi Mungu akamtia Kushan-Rishathaimu mfalme wa Mesopotamia mikononi mwa Othnieli, naye akamshinda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Roho ya Bwana ikamjilia juu yake, naye akawa mwamuzi wa Israeli; akatoka kwenenda vitani, naye Bwana akamtia huyo Kushan-rishathaimu, mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake; na mkono wake ukamshinda Kushan-rishathaimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Othnieli, naye akawa mwamuzi wa Waisraeli. Othnieli alikwenda vitani naye Mwenyezi-Mungu akamtia Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia mikononi mwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Roho wa BWANA akaja juu yake, hivyo akawa mwamuzi wa Israeli, akaenda vitani. BWANA akamtia Kushan-Rishathaimu mfalme wa Aramu mikononi mwa Othnieli, naye akamshinda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Roho wa bwana akaja juu yake, hivyo akawa mwamuzi wa Israeli, akaenda vitani. bwana akamtia Kushan-Rishathaimu mfalme wa Aramu mikononi mwa Othnieli, naye akamshinda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Roho ya BWANA ikamjia juu yake, naye akawa mwamuzi wa Israeli; akatoka kuenda vitani, naye BWANA akamtia huyo Kushan-rishathaimu, mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake; na mkono wake ukamshinda Kushan-rishathaimu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Othnieli, naye akawa mwamuzi wa Waisraeli. Othnieli alikwenda vitani naye Mwenyezi-Mungu akamtia Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia mikononi mwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Roho ya Bwana ilipomjia, akawa mwamuzi wa Waisiraeli, akatoka kwenda vitani, naye Bwana akamtia Kusani-Risataimu, mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake, kwa kuwa mkono wake yeye ulikuwa wenye nguvu kuliko ule wa Kusani-Risataimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Roho ya BWANA ikamjilia juu yake, naye akawa mwamuzi wa Israeli; akatoka kwenenda vitani, naye BWANA akamtia huyo Kushan-rishathaimu, mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake; na mkono wake ukamshinda Kushan-rishathaimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, roho wa Yawe akamujaza Otinieli, naye akakuwa mwamuzi wa Waisraeli. Otinieli alikwenda katika vita naye Yawe akamutia Kusani, Yule-Mwovu-Sana, ufalme wa Mesopotamia, katika mikono yake.