Judges 3:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ehudi akajitengenezea upanga wenye makali kuwili; urefu wake sentimita hamsini. Akaufunga kiunoni mwake upande wa kulia ndani ya mavazi yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Ehudi alikuwa ametengeneza upanga ukatao kuwili, ukiwa na urefu wa kama dhiraa moja, naye akaufunga upanga huo ndani ya nguo yake, kwenye paja lake la mkono wa kuume.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ehudi alijifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wake ulipata dhiraa moja; akaufunga huo upanga ndani ya nguo yake katika paja lake la mkono wa kuume.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ehudi akajitengenezea upanga wenye makali kuwili; urefu wake sentimita hamsini. Akaufunga kiunoni mwake upande wa kulia ndani ya mavazi yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Ehudi alikuwa ametengeneza upanga wenye makali kuwili, urefu wake ni kama dhiraa moja, akaufunga upanga huo ndani ya nguo yake kwenye paja lake la mkono wa kuume.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Ehudi alikuwa ametengeneza upanga wenye ukatao kuwili, urefu wake ni kama dhiraa moja, akaufunga upanga huo ndani ya nguo yake kwenye paja lake la mkono wa kuume.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ehudi alijifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wake ulipata dhiraa moja; akaufunga huo upanga ndani ya nguo yake katika paja lake la mkono wa kulia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ehudi akajitengenezea upanga wenye makali kuwili; urefu wake sentimita hamsini. Akaufunga kiunoni mwake upande wa kulia ndani ya mavazi yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ehudu akajipatia upanga wenye ukali pande zote mbili, nao urefu wake kama mkono; akaufunga chini ya nguo yake penye paja lake la kuume.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ehudi alijifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wake ulipata dhiraa moja; akaufunga huo upanga ndani ya nguo yake katika paja lake la mkono wa kuume.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ehudu akajitengenezea upanga wenye makali ngambo mbili; urefu wake sentimetre makumi tano. Akaufunga kwenye kiuno chake upande wa kuume ndani ya nguo yake.