Judges 3:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ehudi alipoondoka, watumishi wa mfalme wakarudi. Walipoona milango yote ya chumba imefungwa, walifikiri amekwenda kujisaidia chooni humo ndani ya nyumba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada yake kuondoka, watumishi wakaja na kupata milango ya chumba cha juu imefungwa kwa funguo. Wakasema, “Bila shaka anajisaidia chumba cha ndani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi alipokuwa amekwisha toka nje, hao watumishi wake wakaenda; wakaona, na tazama, hiyo milango ya chumba ilikuwa imefungwa kwa ufunguo; nao wakasema, Hapana budi amejifunika miguu yake ndani ya chumba cha baridi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ehudi alipoondoka, watumishi wa mfalme wakarudi. Walipoona milango yote ya chumba imefungwa, walifikiri amekwenda kujisaidia chooni humo ndani ya nyumba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kuondoka, watumishi wakaja na kukuta milango ya chumba cha juu imefungwa kwa funguo. Wakasema, “Bila shaka amejipumzisha kwenye chumba cha ndani cha nyumba yake ya majira ya kiangazi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kuondoka, watumishi wakaja na kukuta milango ya chumba cha juu imefungwa kwa funguo. Wakasema, “Bila shaka amejipumzisha kwenye chumba cha ndani cha nyumba yake ya majira ya kiangazi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi alipokuwa amekwisha toka nje, hao watumishi wake wakaenda; wakaona, na tazama, hiyo milango ya chumba ilikuwa imefungwa kwa ufunguo; nao wakasema, Hapana budi ameenda haja ndani ya chumba cha baridi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ehudi alipoondoka, watumishi wa mfalme wakarudi. Walipoona milango yote ya chumba imefungwa, walifikiri amekwenda kujisaidia chooni humo ndani ya nyumba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokwisha kutoka, watumishi wake Egloni wakaja; lakini walipoona, ya kuwa milango ya chumba cha juu imefungwa kwa makomeo, wakasema; Labda amejifunika miguu yake katika chumba cha baridi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi alipokuwa amekwisha toka nje, hao watumishi wake wakaenda; wakaona, na tazama, hiyo milango ya chumba ilikuwa imefungwa kwa ufunguo; nao wakasema, Hapana budi amejifunika miguu yake ndani ya chumba cha baridi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ehudu alipoondoka, watumishi wa mufalme wakarudi. Walipoona milango yote ya chumba imefungwa, wakafikiri kwamba amekwenda kujisaidia kwenye choo mule ndani ya nyumba.