Judges 3:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipofika huko alipiga tarumbeta katika nchi ya milima ya Efraimu, nao Waisraeli wakateremka pamoja naye kutoka huko milimani naye akawatangulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipofika huko, akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakateremka pamoja naye kutoka vilimani, yeye akiwa anawaongoza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, hapo alipofika akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, ndipo wana wa Israeli wakatelemka pamoja naye kutoka huko milimani, naye akawatangulia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipofika huko alipiga tarumbeta katika nchi ya milima ya Efraimu, nao Waisraeli wakateremka pamoja naye kutoka huko milimani naye akawatangulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipofika huko, akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakatelemka pamoja naye kutoka vilimani, yeye akiwa anawaongoza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipofika huko, akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakateremka pamoja naye kutoka vilimani, yeye akiwa anawaongoza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, hapo alipofika akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, ndipo wana wa Israeli wakateremka pamoja naye kutoka huko milimani, naye akawatangulia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipofika huko alipiga tarumbeta katika nchi ya milima ya Efraimu, nao Waisraeli wakateremka pamoja naye kutoka huko milimani naye akawatangulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoingia humo akapiga baragumu milimani kwa Efuraimu; ndipo, wana wa Isiraeli waliposhuka pamoja naye kutoka milimani, naye akawaongoza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, hapo alipofika akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, ndipo wana wa Israeli wakatelemka pamoja naye kutoka huko milimani, naye akawatangulia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipofika kule akapiga baragumu katika inchi ya milima ya Efuraimu, nao Waisraeli wakateremuka pamoja naye kutoka kule kwenye milima naye akawatangulia.