Judges 3:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akawaambia, “Mnifuate, maana Mwenyezi-Mungu amewatia adui zenu Wamoabu mikononi mwenu.” Wakamfuata mpaka kivuko cha Yordani na kukiteka toka mikononi mwa Wamoabu, wakazuia mtu yeyote kupita.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaagiza, “Nifuateni, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewatia Moabu, adui zenu, mikononi mwenu.” Kwa hiyo wakateremka wakamfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kuelekea Moabu, wala hawakumwacha mtu yeyote kuvuka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Niandameni mimi; kwa kuwa Bwana amewatia adui zenu, Wamoabi, mikononi mwenu. Basi wakatelemka na kumfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha Wamoabi, wala hawakumwacha mtu kuvuka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akawaambia, “Mnifuate, maana Mwenyezi-Mungu amewatia adui zenu Wamoabu mikononi mwenu.” Wakamfuata mpaka kivuko cha Yordani na kukiteka toka mikononi mwa Wamoabu, wakazuia mtu yeyote kupita.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaagiza, “Nifuateni, kwa kuwa BWANA amewatia Moabu, adui zenu, mikononi mwenu.” Kwa hiyo wakatelemka wakamfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kuelekea Moabu, wala hawakuacha mtu ye yote kuvuka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaagiza, “Nifuateni, kwa kuwa bwana amewatia Moabu, adui zenu, mikononi mwenu.” Kwa hiyo wakateremka wakamfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kuelekea Moabu, wala hawakuacha mtu yeyote kuvuka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Nifuateni; kwa kuwa BWANA amewatia adui zenu, Wamoabi, mikononi mwenu. Basi wakateremka na kumfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha Wamoabi, wala hawakumwacha mtu kuvuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akawaambia, “Mnifuate, maana Mwenyezi-Mungu amewatia adui zenu Wamoabu mikononi mwenu.” Wakamfuata mpaka kivuko cha Yordani na kukiteka toka mikononi mwa Wamoabu, wakazuia mtu yeyote kupita.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia: Nifuateni upesi! Kwani Bwana amewatia adui zenu, hawa Wamoabu, mikononi mwenu. Ndipo, waliposhuka na kumfuata, wakavivuka vivuko vya Yordani penye njia za kwenda Moabu, kisha hawakumpa mtu ruhusa kuvuka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Niandameni mimi; kwa kuwa BWANA amewatia adui zenu, Wamoabi, mikononi mwenu. Basi wakatelemka na kumfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha Wamoabi, wala hawakumwacha mtu kuvuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akawaambia: “Munifuate, maana Yawe amewatia waadui zenu Wamoabu katika mikono yenu.” Wakamufuata mpaka kwenye kivuko cha Yordani na kukiteka toka katika mikono ya Wamoabu, wakazuia mutu yeyote kupita.