Judges 3:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli wakamlilia Mwenyezi-Mungu, naye akawapelekea mtu wa kuwakomboa yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli walipomlilia Mwenyezi Mungu, yeye akawainulia mkombozi, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu, ambaye aliwaokoa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wana wa Israeli walipomlingana Bwana, Bwana akawainulia wana wa Israeli mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli wakamlilia Mwenyezi-Mungu, naye akawapelekea mtu wa kuwakomboa yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipomlilia BWANA, yeye akawainulia mwokozi, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu, ambaye aliwaokoa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli walipomlilia bwana, yeye akawainulia mwokozi, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu, ambaye aliwaokoa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wana wa Israeli walipomlilia BWANA, BWANA akawainulia wana wa Israeli mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli wakamlilia Mwenyezi-Mungu, naye akawapelekea mtu wa kuwakomboa yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Isiraeli walipomlilia Bwana, Bwana akawainulia wana wa Isiraeli mwokozi, awaokoe, ndiye Otinieli, mwana wa Kenazi, mdogo wake Kalebu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wana wa Israeli walipomlingana BWANA, BWANA akawainulia wana wa Israeli mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli wakamulilia Yawe, naye akawapelekea mutu wa kuwakomboa, ni kusema Otinieli mwana wa Kenazi, ndugu mudogo wa Kalebu.