Judges 4:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baraki akalifuatia jeshi hilo na magari mpaka Harosheth-hagoimu na kuwaua wanajeshi wote wa Sisera kwa mapanga; hakubaki hata mtu mmoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Baraka akafuata magari ya vita pamoja na jeshi hadi Haroshethi-Hagoyimu. Jeshi lote la Sisera likaanguka kwa upanga, wala hakuna hata mtu mmoja aliyesalia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Baraka akayafuatia magari, na jeshi, hata Haroshethi wa Mataifa; na hilo jeshi lote la Sisera likaanguka kwa makali ya upanga; hakusalia hata mtu mmoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baraki akalifuatia jeshi hilo na magari mpaka Harosheth-hagoimu na kuwaua wanajeshi wote wa Sisera kwa mapanga; hakubaki hata mtu mmoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Baraka akafuatia magari pamoja na jeshi mpaka Haroshethi-Hagoyimu. Jeshi lote la Sisera likaanguka kwa upanga, wala hakuna hata mtu mmoja aliyesalia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Baraka akafuata magari pamoja na jeshi mpaka Haroshethi-Hagoyimu. Jeshi lote la Sisera likaanguka kwa upanga, wala hakuna hata mtu mmoja aliyesalia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Baraka akayafuatia magari, na jeshi, hadi Haroshethi wa Mataifa; na hilo jeshi lote la Sisera likaanguka kwa makali ya upanga; hakusalia hata mtu mmoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baraki akalifuatia jeshi hilo na magari mpaka Harosheth-hagoimu na kuwaua wanajeshi wote wa Sisera kwa mapanga; hakubaki hata mtu mmoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Baraka akayafuata mbiombio magari na majeshi mpaka Haroseti wa Wamizimu; ndiko, hayo majeshi yote ya Sisera walikopigwa kwa ukali wa panga, hakusalia hata mmoja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Baraka akayafuatia magari, na jeshi, hata Haroshethi wa Mataifa; na hilo jeshi lote la Sisera likaanguka kwa makali ya upanga; hakusalia hata mtu mmoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Baraka akawafuatilia waaskari wale na magari mpaka Haroseti-Hagoimu na kuwaua waaskari wote wa Sisera kwa mapanga. Hakukubaki hata mutu mumoja.