Judges 4:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yaeli, mke wa Heberi, akachukua kigingi cha hema na nyundo, akamwendea polepole akakipigilia kile kigingi cha hema katika paji la uso wake kikapenya mpaka udongoni, kwa maana alikuwa amelala fofofo kwa uchovu. Basi, Sisera akafa papo hapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akachukua nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akiwa amelala usingizi kwa kuchoka. Akakipigilia kile kigingi kwenye paji la uso wake, kikapenya hata kuingia ardhini, naye akafa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yaeli, mke wa Heberi, akachukua kigingi cha hema na nyundo, akamwendea polepole akakipigilia kile kigingi cha hema katika paji la uso wake kikapenya mpaka udongoni, kwa maana alikuwa amelala fofofo kwa uchovu. Basi, Sisera akafa papo hapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akachukua nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akiwa amelala usingizi, akiwa amechoka. Akakigongomea kile kigingi kwenye paji la uso wake, kikapenya hata kuingia ardhini, naye akafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akachukua nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akiwa amelala usingizi, akiwa amechoka. Akakigongomea kile kigingi kwenye paji la uso wake, kikapenya hata kuingia ardhini, naye akafa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yaeli, mke wa Heberi, akachukua kigingi cha hema na nyundo, akamwendea polepole akakipigilia kile kigingi cha hema katika paji la uso wake kikapenya mpaka udongoni, kwa maana alikuwa amelala fofofo kwa uchovu. Basi, Sisera akafa papo hapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yaeli, mkewe Heberi, akachukua uwambo mmoja wa hema, akatwaa nayo nyundo mkononi mwake, akamjia polepole, akaupigilia ule uwambo pajini kichwani, mpaka uingie mchangani, maana alikuwa amelala usingizi kabisa; ndipo, alipozimia, akafa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yaeli, muke wa Heberi, akatwaa musumari wa kufungia hema na nyundo, akamwendea polepole akaupigilia ule musumari wa kufungia hema katika paji la uso wake ukapenya mpaka katika udongo, kwa maana alikuwa amelala usingizi muzito sababu ya muchoko. Basi, Sisera akakufa palepale.