Judges 4:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Debora alikuwa na mazoea ya kuketi chini ya mtende uliokuwa kati ya mji wa Rama na mji wa Betheli katika nchi ya milima ya Efraimu. Watu wa Israeli walimjia ili awaamulie mashauri yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Debora alikuwa akiketi chini ya Mtende wa Debora uliokuwa kati ya Rama na Betheli katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakaja kwake ili awaamue.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Debora alikuwa na mazoea ya kuketi chini ya mtende uliokuwa kati ya mji wa Rama na mji wa Betheli katika nchi ya milima ya Efraimu. Watu wa Israeli walimjia ili awaamulie mashauri yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Debora alikuwa akiketi chini ya Mtende wa Debora uliokuwa kati ya Rama na Betheli katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakaja kwake ili awaamue.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Debora alikuwa akiketi chini ya Mtende wa Debora uliokuwa kati ya Rama na Betheli katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakaja kwake ili awaamue.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alikuwa akikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Debora alikuwa na mazoea ya kuketi chini ya mtende uliokuwa kati ya mji wa Rama na mji wa Betheli katika nchi ya milima ya Efraimu. Watu wa Israeli walimjia ili awaamulie mashauri yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyu Debora alikaa chini ya mtende wake katikati ya Rama na Beteli milimani kwa Efuraimu, nao wana wa Isiraeli wakapanda kuja kwake kuamuliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Debora alikuwa anazoea kuikaa chini ya muti wa ngazi uliokuwa kati ya muji wa Rama na muji wa Beteli katika inchi ya milima ya Efuraimu. Watu wa Israeli walimufikia kusudi awaamulie mashauri yao.