Judges 4:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja alimwita Baraki mwana wa Abinoamu wa Kedeshi katika nchi ya Naftali. Alipokuja alimwambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anakuamuru hivi: ‘Nenda ukusanye watu wako mlimani Tabori, uchague watu 10,000 kutoka makabila ya Naftali na Zebuluni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akatuma wamwite Baraka mwana wa Abinoamu kutoka Kedeshi huko Naftali na kumwambia, “Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, anakuagiza: ‘Nenda, chukua wanaume elfu kumi toka Naftali na Zabuloni, mwende Mlima Tabori.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu toka Kedesh-Naftali, akamwambia, Je! Bwana, Mungu wa Israeli, hakutoa amri, akisema, Enenda, ukawavute kwako, huko katika mlima wa Tabori, watu elfu kumi wa wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja alimwita Baraki mwana wa Abinoamu wa Kedeshi katika nchi ya Naftali. Alipokuja alimwambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anakuamuru hivi: ‘Nenda ukusanye watu wako mlimani Tabori, uchague watu 10,000 kutoka makabila ya Naftali na Zebuluni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akatuma wamwite Baraka mwana wa Abinoamu kutoka Kedeshi huko Naftali na kumwambia, “BWANA, Mungu wa Israeli, anakuagiza: ‘Nenda, chukua wanaume 10,000 toka Naftali na Zabuloni, mwende Mlima Tabori.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akatuma wamwite Baraka mwana wa Abinoamu kutoka Kedeshi huko Naftali na kumwambia, “ bwana, Mungu wa Israeli, anakuagiza: ‘Nenda, chukua wanaume 10,000 toka Naftali na Zabuloni, mwende Mlima Tabori.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku moja Debora akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu kutoka Kedesh-Naftali, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli anakuamuru hivi: “Nenda, ukawaogoze watu elfu kumi na wana wa Naftali, na wana wa Zabuloni, ili washike doria katika mlima Tabori”.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja alimwita Baraki mwana wa Abinoamu wa Kedeshi katika nchi ya Naftali. Alipokuja alimwambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anakuamuru hivi: ‘Nenda ukusanye watu wako mlimani Tabori, uchague watu 10,000 kutoka makabila ya Naftali na Zebuluni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akatuma kumwita Baraka, mwana wa Abinoamu wa Kedesi katika nchi ya Nafutali, akamwambia: Bwana Mungu wa Isiraeli hakukuagiza: Nenda kushika njia ya kwenda mlimani kwa Tabori, uchukue kwao wana wa Nafutali nako kwao wana wa Zebuluni watu 10000 wa kwenda na wewe?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu toka Kedesh-Naftali, akamwambia, Je! BWANA, Mungu wa Israeli, hakutoa amri, akisema, Enenda, ukawavute kwako, huko katika mlima wa Tabori, watu elfu kumi wa wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja akamwita Baraka mwana wa Abinoamu wa Kedesi katika inchi ya Nafutali. Alipokuja akamwambia: “Yawe, Mungu wa Israeli, anakuamuru hivi: ‘Kwenda ukusanye watu wako kwenye mulima Tabori, uchague watu elfu kumi kutoka makabila ya Nafutali na Zebuluni.