Judges 5:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mashujaa waliobaki waliteremka, watu wa Mwenyezi-Mungu walikwenda kumpigania dhidi ya wenye nguvu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ndipo mabaki ya watu wakashuka dhidi ya wakuu, watu wa Mwenyezi Mungu wakashuka kwangu dhidi ya wenye nguvu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo walitelemka mabaki ya waungwana na ya watu; Bwana alishuka kwa ajili yangu apigane na mashujaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mashujaa waliobaki waliteremka, watu wa Mwenyezi-Mungu walikwenda kumpigania dhidi ya wenye nguvu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ndipo mabaki ya watu wakashuka dhidi ya wenye nguvu, watu wa BWANA, wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ndipo mabaki ya watu wakashuka dhidi ya wenye nguvu, watu wa bwana, wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo waliteremka mabaki ya waungwana na ya watu; BWANA alishuka kwa ajili yangu apigane na mashujaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mashujaa waliobaki waliteremka, watu wa Mwenyezi-Mungu walikwenda kumpigania dhidi ya wenye nguvu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, waliosalia waliposhuka kuwaendea wale watukufu, Bwana naye akashuka kuja kwangu nao hao mafundi wa vita:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo walitelemka mabaki ya waungwana na ya watu; BWANA alishuka kwa ajili yangu apigane na mashujaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mashujaa waliobaki waliteremuka. Watu wa Yawe walikwenda kumupigania na wenye nguvu.