Judges 5:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Malaika wa Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Uapizeni mji wa Merosi, waapizeni vikali wakazi wake; maana hawakuja kumsaidia Mwenyezi-Mungu hawakumsaidia Mwenyezi-Mungu dhidi ya wenye nguvu’.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika wa Mwenyezi Mungu akasema, ‘Laani Merozi. Laani watu wake kwa uchungu, kwa kuwa hawakuja kumsaidia Mwenyezi Mungu, kumsaidia Mwenyezi Mungu dhidi ya hao wenye nguvu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ulaanini Merozi, alisema malaika wa Bwana, Walaanini kwa uchungu wenyeji wake; Kwa maana hawakuja kumsaidia Bwana, Kumsaidia Bwana juu ya hao wenye nguvu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Malaika wa Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Uapizeni mji wa Merosi, waapizeni vikali wakazi wake; maana hawakuja kumsaidia Mwenyezi-Mungu hawakumsaidia Mwenyezi-Mungu dhidi ya wenye nguvu’.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika wa BWANA akasema, ‘Merozi alaaniwe. Walaaniwe watu wake kwa uchungu, kwa kuwa hawakuja kumsaidia BWANA, kumsaidia BWANA dhidi ya hao wenye nguvu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika wa bwana akasema, ‘Merozi alaaniwe. Walaaniwe watu wake kwa uchungu, kwa kuwa hawakuja kumsaidia bwana, kumsaidia bwana dhidi ya hao wenye nguvu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ulaanini Merozi, alisema malaika wa BWANA, Walaanini kwa uchungu wenyeji wake; Kwa maana hawakuja kumsaidia BWANA, Kumsaidia BWANA juu ya hao wenye nguvu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Malaika wa Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Uapizeni mji wa Merosi, waapizeni vikali wakazi wake; maana hawakuja kumsaidia Mwenyezi-Mungu hawakumsaidia Mwenyezi-Mungu dhidi ya wenye nguvu’.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo malaika wa Bwana: Uapizeni Merozi! Waapizeni! Waapizeni wao wenyeji wake! Kwani hawakufika kusaidiana na Bwana, hawakusaidiana na Bwana kwao walio mafundi wa vita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ulaanini Merozi, alisema malaika wa BWANA, Walaanini kwa uchungu wenyeji wake; Kwa maana hawakuja kumsaidia BWANA, Kumsaidia BWANA juu ya hao wenye nguvu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Malaika wa Yawe anasema hivi: ‘Ulaani muji wa Merosi, uwalaani vikali wakaaji wake; maana hawakukuja kumusaidia Yawe hawakumusaidia Yawe juu ya wenye nguvu’.