Judges 5:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ee Mwenyezi-Mungu, waangamie adui zako wote! Lakini rafiki zako na wawe kama jua, wakati linapochomoza kwa mwanga mkubwa!” Nayo nchi ikawa na amani kwa muda wa miaka arubaini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Adui zako wote na waangamie hivyo, Ee Mwenyezi Mungu! Bali wote wanaokupenda na wawe kama jua linavyochomoza kwa nguvu zake.” Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na waangamie vivyo hivyo adui zako wote, Ee Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ee Mwenyezi-Mungu, waangamie adui zako wote! Lakini rafiki zako na wawe kama jua, wakati linapochomoza kwa mwanga mkubwa!” Nayo nchi ikawa na amani kwa muda wa miaka arubaini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Adui zako wote na waangamie, Ee BWANA! Bali wote wakupendao na wawe kama jua lichomozavyo kwa nguvu zake.” Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Adui zako wote na waangamie, Ee bwana! Bali wote wakupendao na wawe kama jua lichomozavyo kwa nguvu zake.” Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na waangamie vivyo hivyo adui zako wote, Ee BWANA. Bali wao wampendao na wawe kama jua hapo litokapo kwa nguvu zake. Nayo nchi ikastarehe miaka arobaini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ee Mwenyezi-Mungu, waangamie adui zako wote! Lakini rafiki zako na wawe kama jua, wakati linapochomoza kwa mwanga mkubwa!” Nayo nchi ikawa na amani kwa muda wa miaka arubaini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo na waangamie wote walio adui zako, Bwana! Lakini wao wampendao na wawe kama jua lenyewe, likija kucha lenye utukufu wake! Kisha nchi ikapata kutulia miaka 40.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na waangamie vivyo hivyo adui zako wote, Ee BWANA. Bali wao wampendao na wawe kama jua hapo litokapo kwa nguvu zake. Nayo nchi ikastarehe miaka arobaini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ee Yawe, waangamie waadui zako wote! Lakini warafiki zako wakuwe kama jua, wakati linapochomoza kwa mwangaza mukubwa!” Inchi ya Waisraeli ikakuwa na amani kwa muda wa miaka makumi ine.