Judges 6:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Malaika wa Mwenyezi-Mungu akaenda, akaketi chini ya mwaloni wa Yoashi, Mwabiezeri, huko Ofra. Gideoni mwana wa Yoashi, alikuwa anapura ngano ndani ya shinikizo la kusindikia zabibu ili Wamidiani wasimwone.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika wa Mwenyezi Mungu akaja akaketi chini ya mwaloni ulio Ofra, ambao ulikuwa mali ya Yoashi Mwabiezeri, pale Gideoni mwanawe alikuwa akipepeta ngano penye shinikizo la kukamulia zabibu, ili kuificha Wamidiani wasiione.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Malaika wa Mwenyezi-Mungu akaenda, akaketi chini ya mwaloni wa Yoashi, Mwabiezeri, huko Ofra. Gideoni mwana wa Yoashi, alikuwa anapura ngano ndani ya shinikizo la kusindikia zabibu ili Wamidiani wasimwone.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika wa BWANA akaja akaketi chini ya mti wa mwaloni huko Ofra, ambao ulikuwa mali ya Yoashi Mwebiezeri, ambako Gideoni mwanawe alikuwa akipepeta ngano penye shinikizo la kukamulia zabibu, ili kuificha Wamidiani wasiione.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika wa bwana akaja akaketi chini ya mti wa mwaloni huko Ofra, ambao ulikuwa mali ya Yoashi, Mwabiezeri, ambako Gideoni mwanawe alikuwa akipepeta ngano penye shinikizo la kukamulia zabibu, ili kuificha Wamidiani wasiione.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Malaika wa BWANA akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwaabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Malaika wa Mwenyezi-Mungu akaenda, akaketi chini ya mwaloni wa Yoashi, Mwabiezeri, huko Ofra. Gideoni mwana wa Yoashi, alikuwa anapura ngano ndani ya shinikizo la kusindikia zabibu ili Wamidiani wasimwone.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha malaika wa Bwana akaja, akakaa chini ya mkwaju kule Ofura uliokuwa wa Yoasi wa Abiezeri, mwanawe Gideoni alipokuwa akipura ngano penye kukamulia mvinyo, azifiche machoni pa Wamidiani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Malaika wa BWANA akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Malaika wa Yawe akaenda, akaikaa chini ya muti wa mwalo wa Yoasi Mwabiezeri, kule Ofura. Gideoni mwana wa Yoasi alikuwa anapepeta ngano ndani ya kikamulio cha kukamulia zabibu kusudi Wamidiani wasimwone.