Judges 6:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Gideoni akamwambia, “Ee Bwana wangu, ikiwa Mwenyezi-Mungu yuko pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu ambayo wazee wetu walitusimulia, wakisema: ‘Mwenyezi-Mungu ndiye aliyetutoa nchini Misri.’ Lakini sasa Mwenyezi-Mungu ametutupa na kututia mikononi mwa Wamidiani!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Gideoni akajibu, “Nisamehe, Ee Bwana wangu. Kama Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi yale matendo yake makuu ambayo baba zetu walitusimulia juu yake waliposema, ‘Je, Mwenyezi Mungu hakutupandisha kutoka Misri?’ Lakini sasa Mwenyezi Mungu ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye Bwana, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Gideoni akamwambia, “Ee Bwana wangu, ikiwa Mwenyezi-Mungu yuko pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu ambayo wazee wetu walitusimulia, wakisema: ‘Mwenyezi-Mungu ndiye aliyetutoa nchini Misri.’ Lakini sasa Mwenyezi-Mungu ametutupa na kututia mikononi mwa Wamidiani!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Gideoni akajibu, “Ee Bwana wangu, kama BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi basi yale matendo yake makuu baba zetu waliyotusimulia juu yake waliposema, ‘Je, BWANA hakutupandisha kutoka Misri?’ Lakini sasa BWANA ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Gideoni akajibu, “Ee Bwana wangu, kama bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi basi yale matendo yake makuu baba zetu waliyotusimulia juu yake waliposema, ‘Je, bwana hakutupandisha kutoka Misri?’ Lakini sasa bwana ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Wamidiani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Gideoni akamwambia, “Ee Bwana wangu, ikiwa Mwenyezi-Mungu yuko pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu ambayo wazee wetu walitusimulia, wakisema: ‘Mwenyezi-Mungu ndiye aliyetutoa nchini Misri.’ Lakini sasa Mwenyezi-Mungu ametutupa na kututia mikononi mwa Wamidiani!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Gideoni akamwambia: E bwana wangu, kama Bwana yuko nasi, haya yote yamewezaje kutupata? Yako wapi matendo yake yote ya kustaajabu, baba zetu waliyotusimulia kwamba: Kumbe Bwana hakutuleta huku na kututoa Misri? Lakini sasa Bwana ametutupa, akatutia mikononi mwa Wamidiani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Gideoni akamwambia: “Ee Bwana wangu, ikiwa Yawe yuko pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu ambayo wazee wetu walituelezea, wakisema: ‘Yawe ndiye aliyetutoa katika inchi ya Misri.’ Lakini sasa Yawe ametutupilia na kututia katika mikono ya Wamidiani!”