Judges 6:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Gideoni akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu huko na kuyaita, “Mwenyezi-Mungu ni Amani.” Madhabahu hiyo iko huko Ofra, mji wa Wabiezeri, mpaka leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Gideoni akamjengea Mwenyezi Mungu madhabahu mahali pale na kupaita Yehova-Shalomu. Hata leo imesimama huko Ofra ya Waabiezeri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Gideoni akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu huko na kuyaita, “Mwenyezi-Mungu ni Amani.” Madhabahu hiyo iko huko Ofra, mji wa Wabiezeri, mpaka leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu mahali pale na kupaita, Yehova-Shalom. Mpaka leo ingalipo imesimama huko Ofra ya Waabiezeri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Gideoni akamjengea bwana madhabahu mahali pale na kupaita, Yehova-Shalom. Mpaka leo ingalipo imesimama huko Ofra ya Waabiezeri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Gideoni akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu huko na kuyaita, “Mwenyezi-Mungu ni Amani.” Madhabahu hiyo iko huko Ofra, mji wa Wabiezeri, mpaka leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Gideon akamjengea Bwana huko pa kumtambikia, akapaita Utengemano wa Bwana, napo pangalipo hata siku hii ya leo huko Ofura kwao wa Abiezeri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Gideoni akamujengea Yawe mazabahu kule na kuyaita, “Yawe ni Amani.” Mazabahu hiyo iko kule Ofura, muji wa Waabiezeri, mpaka leo.