Judges 6:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Usiku huo, Mwenyezi-Mungu akamwambia Gideoni, “Chukua fahali mmoja wa baba yako, fahali yule wa pili wa umri wa miaka saba. Bomoa madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako na kuvunja sanamu ya Ashera iliyo karibu nayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Usiku ule ule Mwenyezi Mungu akamwambia, “Mchukue ng’ombe dume wa baba yako, yule wa pili mwenye miaka saba, ubomoe madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako, na ukaikate nguzo ya Ashera iliyo karibu nayo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Usiku huo, Mwenyezi-Mungu akamwambia Gideoni, “Chukua fahali mmoja wa baba yako, fahali yule wa pili wa umri wa miaka saba. Bomoa madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako na kuvunja sanamu ya Ashera iliyo karibu nayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Usiku ule ule BWANA akamwambia, “Mchukue ng'ombe dume wa baba yako, yaani, yule wa pili mwenye miaka saba, na ubomoe ile madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako, na ukaikate ile Ashera iliyo karibu nayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Usiku ule ule bwana akamwambia, “Mchukue ng’ombe dume wa baba yako, yaani, yule wa pili mwenye miaka saba, na ubomoe madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako, na ukaikate Ashera iliyo karibu nayo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa usiku huo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Usiku huo, Mwenyezi-Mungu akamwambia Gideoni, “Chukua fahali mmoja wa baba yako, fahali yule wa pili wa umri wa miaka saba. Bomoa madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako na kuvunja sanamu ya Ashera iliyo karibu nayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa usiku ule, ndipo, Bwana alipomwambia: Chukua dume la ng'ombe la baba yako na dume jingine la ng'ombe la miaka saba! Kisha pabomoe mahali pa baba yako pa kumtambikia Baali, nacho kinyago cha Ashera kilichopo hapohapo kando yake kikatekate!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng’ombe wa baba yako, yaani ng’ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usiku ule, Yawe akamwambia Gideoni: “Twaa ngombe dume mumoja wa baba yako, ngombe dume yule wa pili wa umri wa miaka saba. Bomoa mazabahu ya mungu Bali baba yako anayokuwa nayo na kuvunja sanamu ya mungu Ashera inayokuwa karibu nayo.