Judges 6:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu, unijengee mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, madhabahu nzuri juu ya mwinuko huu. Kisha unitolee sadaka ya kuteketezwa ya yule fahali wa pili ukitumia kuni za ile sanamu ya Ashera uliyoivunja.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha mjengee Mwenyezi Mungu, Mungu wako, madhabahu kwa taratibu zake juu ya mwamba katika ngome hii. Kwa kutumia kuni za hiyo nguzo ya Ashera uliyoikatakata, mtoe sadaka huyo dume wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu, unijengee mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, madhabahu nzuri juu ya mwinuko huu. Kisha unitolee sadaka ya kuteketezwa ya yule fahali wa pili ukitumia kuni za ile sanamu ya Ashera uliyoivunja.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha mjengee BWANA Mungu wako, madhabahu halisi, kwa taratibu zake, juu ya huu mwamba. Kwa kutumia kuni za hiyo nguzo ya Ashera uliyoikatakata, mtoe sadaka huyo dume wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha mjengee bwana Mwenyezi Mungu wako, madhabahu halisi, kwa taratibu zake, juu ya huu mwamba. Kwa kutumia kuni za hiyo nguzo ya Ashera uliyoikatakata, mtoe sadaka huyo dume wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ukamjengee BWANA, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu, unijengee mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, madhabahu nzuri juu ya mwinuko huu. Kisha unitolee sadaka ya kuteketezwa ya yule fahali wa pili ukitumia kuni za ile sanamu ya Ashera uliyoivunja.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha umjengee Bwana Mungu wako pa kumtambikia hapa juu ngomeni na kupatengeneza vema! Kisha lichukue lile dume la ng'ombe la pili, ulitoe kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ukivitumia vile vipande vya kinyago cha Ashera, ulichokikatakata, kuwa kuni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ukamjengee BWANA, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng’ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu, unijengee mimi Yawe, Mungu wako, mazabahu nzuri juu ya mwinuko ule. Kisha unitolee sadaka ya kuteketezwa ya yule ngombe dume wa pili ukitumia kuni za ile sanamu ya Ashera uliyoivunja.”