Judges 6:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Gideoni akachukua watumishi wake kumi, akafanya kama alivyoagizwa na Mwenyezi-Mungu. Lakini kwa kuwa aliiogopa jamaa yake na watu wa mjini, badala ya kufanya hayo mchana, alifanya wakati wa usiku.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Gideoni akawachukua watumishi wake kumi na kufanya kama Mwenyezi Mungu alivyomwambia. Lakini kwa kuwa aliwaogopa jamaa yake na watu wa mji, akafanya haya usiku badala ya mchana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama Bwana alivyomwambia; lakini ikawa kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Gideoni akachukua watumishi wake kumi, akafanya kama alivyoagizwa na Mwenyezi-Mungu. Lakini kwa kuwa aliiogopa jamaa yake na watu wa mjini, badala ya kufanya hayo mchana, alifanya wakati wa usiku.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Gideoni akawachukua watumishi wake kumi na kufanya kama BWANA alivyomwambia. Lakini kwa kuwa aliwaogopa jamaa yake na watu wa mji, akafanya haya usiku badala ya mchana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Gideoni akawachukua watumishi wake kumi na kufanya kama bwana alivyomwambia. Lakini kwa kuwa aliwaogopa jamaa yake na watu wa mji, akafanya haya usiku badala ya mchana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama BWANA alivyomwambia; lakini kwa kuwa aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Gideoni akachukua watumishi wake kumi, akafanya kama alivyoagizwa na Mwenyezi-Mungu. Lakini kwa kuwa aliiogopa jamaa yake na watu wa mjini, badala ya kufanya hayo mchana, alifanya wakati wa usiku.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Gideoni alipochukua watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya, kama Bwana alivyomwagiza; lakini kwa kuwaogopa wao wa mlango wa baba yake na watu wa mjini hakuvifanya machana, ila usiku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama BWANA alivyomwambia; lakini ikawa kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Gideoni akatwaa watumishi wake kumi, akafanya kama vile alivyoagizwa na Yawe. Lakini kwa sababu aliiogopa jamaa yake na watu wa muji, pahali pa kufanya hayo muchana, akayafanya wakati wa usiku.