Judges 6:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakazi wa mji walipoamka asubuhi na mapema waliona madhabahu ya Baali na sanamu ya Ashera iliyokuwa karibu nayo vimeharibiwa. Yule fahali wa pili alikuwa ameteketezwa juu ya madhabahu iliyokuwa imejengwa mahali hapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa mji walipoamka asubuhi, tazama madhabahu ya Baali imebomolewa, na nguzo ya Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwakatwa, na yule ng’ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya madhabahu iliyojengwa upya!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata watu wa mji walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakazi wa mji walipoamka asubuhi na mapema waliona madhabahu ya Baali na sanamu ya Ashera iliyokuwa karibu nayo vimeharibiwa. Yule fahali wa pili alikuwa ameteketezwa juu ya madhabahu iliyokuwa imejengwa mahali hapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wa mji walipoamka asubuhi, tazama madhabahu ya Baali imebomolewa na nguzo ya Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwakatwa na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya madhabahu iliyojengwa upya!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa mji walipoamka asubuhi, tazama madhabahu ya Baali imebomolewa na nguzo ya Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwakatwa na yule ng’ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya madhabahu yaliyojengwa upya!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata wakazi wa mji walipoamka asubuhi na mapema, wakaona madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakazi wa mji walipoamka asubuhi na mapema waliona madhabahu ya Baali na sanamu ya Ashera iliyokuwa karibu nayo vimeharibiwa. Yule fahali wa pili alikuwa ameteketezwa juu ya madhabahu iliyokuwa imejengwa mahali hapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wa mjini walipoamka asubuhi na mapema, wakaona: Pa kumtambikia Baali pamebomolewa, nacho kinyago cha Ashera kilichokuwa kando yake kimekatwakatwa, nalo dume la pili limekwisha kuteketezwa lote zima hapo pengine pa kutambikia palipojengwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata watu wa mji walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng’ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaaji wa muji walipoamuka asubui mapema waliona mazabahu ya Bali na sanamu ya Ashera iliyokuwa karibu nayo vimeharibiwa. Yule ngombe dume wa pili alikuwa ameteketezwa juu ya mazabahu iliyokuwa imejengwa pahali pale.