Judges 6:37 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
sasa naweka ngozi ya kondoo kwenye sakafu ya kupuria ngano. Ikiwa kutakuwa na umande juu ya ngozi tu, na sakafu inayoizunguka ikawa kavu, basi, nitajua kuwa utawaokoa Waisraeli kwa mkono wangu kama ulivyosema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
tazama, nitaweka manyoya ya kondoo kwenye sakafu ya kupuria nafaka, na kama utakuwepo umande juu ya manyoya tu, na ardhi yote ikiwa kavu, ndipo nitakapojua kuwa utaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tazama, nitaweka ngozi ya kondoo katika kiwanja cha kupuria; na kama ukiwapo umande juu ya ngozi tu, na nchi yote ikiwa kavu, basi, hapo ndipo nitakapojua ya kuwa utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
sasa naweka ngozi ya kondoo kwenye sakafu ya kupuria ngano. Ikiwa kutakuwa na umande juu ya ngozi tu, na sakafu inayoizunguka ikawa kavu, basi, nitajua kuwa utawaokoa Waisraeli kwa mkono wangu kama ulivyosema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
tazama, nitaweka ngozi ya kondoo kwenye kiwanja cha kupuria nafaka, na kama utakuwepo umande juu ya ngozi tu, nayo ardhi yote ikiwa kavu, ndipo nitakapojua kuwa utaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
tazama, nitaweka ngozi ya kondoo kwenye kiwanja cha kupuria nafaka, na kama utakuwepo umande juu ya ngozi tu, nayo ardhi yote ikiwa kavu, ndipo nitakapojua kuwa utaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, nitaweka ngozi ya kondoo katika kiwanja cha kupuria; na kama ukiwapo umande juu ya ngozi tu, na nchi yote ikiwa kavu, basi, hapo ndipo nitakapojua ya kuwa utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
sasa naweka ngozi ya kondoo kwenye sakafu ya kupuria ngano. Ikiwa kutakuwa na umande juu ya ngozi tu, na sakafu inayoizunguka ikawa kavu, basi, nitajua kuwa utawaokoa Waisraeli kwa mkono wangu kama ulivyosema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
basi, niweke ngozi ya kondoo yenye manyoya hapa penye kupuria ngano; kama umande utakuwa ngozini tu, nchi yote ikiwa kavu, ndipo, nitakapojua, ya kuwa utawaokoa Waisiraeli kwa kuitumia mikono yangu, kama ulivyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tazama, nitaweka ngozi ya kondoo katika kiwanja cha kupuria; na kama ukiwapo umande juu ya ngozi tu, na nchi yote ikiwa kavu, basi, hapo ndipo nitakapojua ya kuwa utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
sasa ninaweka ngozi ya kondoo chini kwenye kiwanja cha kupepetea ngano. Ikiwa kutakuwa umande juu ya ngozi tu, na udongo unaouzunguka ikakuwa mukavu, basi, nitajua kwamba utawaokoa Waisraeli kwa mukono wangu kama ulivyosema.”