Judges 6:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Adui waliozoea kuja kwa wingi kama nzige, pamoja na ng'ombe na ngamia wao na kufanya makao yao nchini Israeli, waliharibu nchi ya Israeli kwa vile walikuwa wengi mno wasiohesabika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipanda na mifugo yao na mahema yao, mfano wa makundi ya nzige. Ilikuwa haiwezekani kuwahesabu watu na ngamia wao; wakavamia nchi ili kuiharibu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana walikwea na ng'ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Adui waliozoea kuja kwa wingi kama nzige, pamoja na ng'ombe na ngamia wao na kufanya makao yao nchini Israeli, waliharibu nchi ya Israeli kwa vile walikuwa wengi mno wasiohesabika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipanda na mifugo yao na mahema yao, mfano wa makundi ya nzige. Ilikuwa haiwezekani kuwahesabu watu na ngamia zao; wakavamia nchi ili kuiharibu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipanda na mifugo yao na mahema yao, mfano wa makundi ya nzige. Ilikuwa haiwezekani kuwahesabu watu na ngamia zao; wakavamia nchi ili kuiharibu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana walikwea na ng'ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Adui waliozoea kuja kwa wingi kama nzige, pamoja na ng'ombe na ngamia wao na kufanya makao yao nchini Israeli, waliharibu nchi ya Israeli kwa vile walikuwa wengi mno wasiohesabika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani walipopanda wakaleta makundi na mahema yao, wakaja wengi mno kama nzige, hawakuhesabika wala wenyewe, wala ngamia wao, nao wakajia tu kuiharibu nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana walikwea na ng’ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waadui waliozoea kuja kwa wingi kama nzige, pamoja na ngombe na ngamia wao na kufanya makao yao katika inchi ya Israeli, waliharibu inchi ya Israeli kwa vile walikuwa wengi sana wasiohesabika.