Judges 7:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Gideoni alipofika, akamsikia mtu mmoja akimsimulia mwenzake ndoto yake hivi: “Niliota ndoto. Niliona mkate wa shayiri ukivingirika hadi kambini mwa Wamidiani, ukalipiga hema na kulipindua chini juu. Hema likalala chini.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Gideoni alifika mara tu mtu mmoja alipokuwa akimweleza mwenzake ndoto yake, akisema, “Tazama, niliota ndoto, mkate wa shayiri ulioviringana ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukaipiga hema kwa nguvu, na kusababisha hema hilo kupinduka na kuporomoka.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata Gideoni alipofika, tazama, palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akimhadithia mwenziwe ndoto, akasema, Tazama, naliota ndoto, na tazama, mkate wa shayiri ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukafika hata hema moja, ukaipiga hata ikaanguka, nao ukaipindua, hata ikalala chini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Gideoni alipofika, akamsikia mtu mmoja akimsimulia mwenzake ndoto yake hivi: “Niliota ndoto. Niliona mkate wa shayiri ukivingirika hadi kambini mwa Wamidiani, ukalipiga hema na kulipindua chini juu. Hema likalala chini.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Gideoni alifika wakati huo huo kukiwa na mtu mmoja aliyekuwa anamweleza mwenzake ndoto yake, akisema, “Niliota ndoto: Tazama mkate wa shayiri ulioviringana ulianguka katika kambi moja ya Wamidiani, ukaipiga na ikaanguka nao ukaipindua juu chini na hema ikaporomoka chini.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Gideoni alifika wakati huo huo kukiwa na mtu mmoja aliyekuwa anamweleza mwenzake ndoto yake, akisema, “Niliota ndoto: Tazama mkate wa shayiri ulioviringana ulianguka katika kambi moja ya Wamidiani, ukaipiga na ikaanguka nao ukaipindua juu chini na hema ikaporomoka chini.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata Gideoni alipofika, tazama, palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akimhadithia mwenziwe ndoto, akasema, Tazama, niliota ndoto, na tazama, mkate wa shayiri ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukafika katika hema moja, ukaipiga hadi ikaanguka, ukaipindua, hadi ikalala chini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Gideoni alipofika, akamsikia mtu mmoja akimsimulia mwenzake ndoto yake hivi: “Niliota ndoto. Niliona mkate wa shayiri ukivingirika hadi kambini mwa Wamidiani, ukalipiga hema na kulipindua chini juu. Hema likalala chini.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Gideoni alipofika, mara akasikia, mtu alivyomsimulia mwenzake ndoto na kusema: Angalia! Nimeota ndoto, nikaona, mkate wa mofa wa mawele ulivyofingirika katika makambi ya Wamidiani, ukafika kwenye hema moja, ukalipiga, lianguke, ukalifudikiza, ya chini yaje juu; basi, hilo hema likalala hivyo pale chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata Gideoni alipofika, tazama, palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akimhadithia mwenziwe ndoto, akasema, Tazama, naliota ndoto, na tazama, mkate wa shayiri ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukafika hata hema moja, ukaipiga hata ikaanguka, nao ukaipindua, hata ikalala chini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Gideoni alipofika, akamusikia mutu mumoja akisimulia na mwenzake juu ya ndoto yake hivi: “Niliota ndoto. Nikaona mukate wa shayiri ukiviringikaviringika mpaka katika kambi ya Wamidiani, ukalipiga hema na kulipindua machali juu. Hema likalala chini.”