Judges 7:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitakapopiga tarumbeta, mimi pamoja na kundi langu, nyote pigeni tarumbeta kutoka kila upande na kusema kwa sauti kubwa, ‘Kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu na kwa ajili ya Gideoni!’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi na wote walio pamoja nami tutakapopiga tarumbeta zetu, ninyi nanyi pigeni tarumbeta pande zote za kambi na mpige kelele, mseme, ‘Upanga wa Mwenyezi Mungu na wa Gideoni.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nitakapopiga tarumbeta, mimi na wote walio pamoja nami, basi ninyi nanyi zipigeni tarumbeta pande zote za kambi, mkaseme, Kwa Bwana, na kwa Gideoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitakapopiga tarumbeta, mimi pamoja na kundi langu, nyote pigeni tarumbeta kutoka kila upande na kusema kwa sauti kubwa, ‘Kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu na kwa ajili ya Gideoni!’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mimi na wale walio pamoja nami wote, tutakapopiga tarumbeta zetu, ninyi nanyi pigeni tarumbeta pande zote za kambi na mpige kelele, mseme, ‘Upanga wa BWANA na wa Gideoni.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati mimi na wale walio pamoja nami wote, tutakapopiga tarumbeta zetu, ninyi nanyi pigeni tarumbeta pande zote za kambi na mpige kelele, mseme, ‘Upanga wa bwana na wa Gideoni.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nitakapopiga tarumbeta, mimi na wote walio pamoja nami, basi ninyi nanyi zipigeni tarumbeta pande zote za kambi, mkaseme, Kwa BWANA, na kwa Gideoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitakapopiga tarumbeta, mimi pamoja na kundi langu, nyote pigeni tarumbeta kutoka kila upande na kusema kwa sauti kubwa, ‘Kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu na kwa ajili ya Gideoni!’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitakapopiga baragumu mimi pamoja nao wote walioko kwangu, ndipo, nanyi mtakapoyapiga mabaragumu pande zote pia za makambi yote na kusema: Tunaye Bwana na Gideoni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nitakapopiga tarumbeta, mimi na wote walio pamoja nami, basi ninyi nanyi zipigeni tarumbeta pande zote za kambi, mkaseme, Kwa BWANA, na kwa Gideoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitakapopiga baragumu, mimi pamoja na kundi langu, ninyi wote mupige baragumu kutoka kila upande na kusema kwa sauti kubwa: ‘Kwa ajili ya Yawe na kwa ajili ya Gideoni!’ ”