Judges 7:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makundi yote matatu kwa pamoja yakapiga tarumbeta na kuvunja magudulia yao. Katika mikono yao ya kushoto walishika mienge na kwa mikono yao ya kulia tarumbeta na kuzipiga, huku wakisema kwa sauti kubwa, “Upanga kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu na kwa ajili ya Gideoni!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yale makundi matatu wakapiga tarumbeta na kuvunja mitungi. Wakashika mienge kwa mikono yao ya kushoto, na tarumbeta katika mikono yao ya kuume ili kuzipiga. Wakapaza sauti zao, wakisema, “Upanga wa Mwenyezi Mungu, na wa Gideoni!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vile vikosi vitatu wakapiga tarumbeta, wakaivunja mitungi, wakaishika mienge kwa mikono yao ya kushoto, na zile tarumbeta katika mikono yao ya kuume ili kuzipiga; wakapiga kelele, Upanga wa Bwana na wa Gideoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makundi yote matatu kwa pamoja yakapiga tarumbeta na kuvunja magudulia yao. Katika mikono yao ya kushoto walishika mienge na kwa mikono yao ya kulia tarumbeta na kuzipiga, huku wakisema kwa sauti kubwa, “Upanga kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu na kwa ajili ya Gideoni!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yale makundi matatu yakapiga tarumbeta na kuvunja mitungi. Wakashika mienge kwa mikono yao ya kushoto na katika mikono yao ya kuume tarumbeta ili kuzipiga, wakapaza sauti zao, “Upanga wa BWANA na wa Gideoni!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yale makundi matatu yakapiga tarumbeta na kuvunja mitungi. Wakashika mienge kwa mikono yao ya kushoto na katika mikono yao ya kuume tarumbeta ili kuzipiga, wakapaza sauti zao, “Upanga wa bwana na wa Gideoni!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Vile vikosi vitatu wakapiga tarumbeta, wakaivunja mitungi, wakaishika mienge kwa mikono yao ya kushoto, na zile tarumbeta katika mikono yao ya kulia ili kuzipiga; wakapiga kelele, Upanga wa BWANA na wa Gideoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makundi yote matatu kwa pamoja yakapiga tarumbeta na kuvunja magudulia yao. Katika mikono yao ya kushoto walishika mienge na kwa mikono yao ya kulia tarumbeta na kuzipiga, huku wakisema kwa sauti kubwa, “Upanga kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu na kwa ajili ya Gideoni!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, vikosi vyote vitatu vilipoyapiga mabaragumu na kuvivunja vile vyungu, wakashika mikononi mwao mwa kushoto mienge, namo mikononi mwao mwa kulia yale mabaragumu ya kupiga, wakapiga makelele kwamba: Tunao upanga wa Bwana na wa Gideoni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vile vikosi vitatu wakapiga tarumbeta, wakaivunja mitungi, wakaishika mienge kwa mikono yao ya kushoto, na zile tarumbeta katika mikono yao ya kuume ili kuzipiga; wakapiga kelele, Upanga wa BWANA na wa Gideoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makundi yote matatu kwa pamoja yakapiga baragumu na kuvunja mitungi yao. Katika mikono yao ya kushoto walishika mienge na kwa mikono yao ya kuume baragumu na kuzipiga, na walikuwa wanasema kwa sauti kubwa: “Upanga kwa ajili ya Yawe na kwa ajili ya Gideoni!”