Judges 7:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Gideoni walipopiga tarumbeta zao 300, Mwenyezi-Mungu aliwafanya Wamidiani waanze kuuana wao kwa wao kambini. Waliosalia wakatoroka hadi Serera panapoelekea Beth-shita, hadi mpakani mwa Abel-mehola karibu na Tabathi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipozipiga zile tarumbeta mia tatu, Mwenyezi Mungu akafanya watu katika kambi yote kugeukiana kila mmoja na mwenziwe kwa upanga. Jeshi likakimbia hadi Beth-Shita kuelekea Serera, hadi mpakani mwa Abel-Mehola karibu na Tabathi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakazipiga zile tarumbeta mia tatu, naye Bwana akaufanya upanga wa kila mtu uwe juu ya mwenziwe, na juu ya jeshi lote, jeshi likakimbia mpaka Bethshita, kuendelea Serera, hata mpaka wa Abel-Mehola, karibu na Tabathi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Gideoni walipopiga tarumbeta zao 300, Mwenyezi-Mungu aliwafanya Wamidiani waanze kuuana wao kwa wao kambini. Waliosalia wakatoroka hadi Serera panapoelekea Beth-shita, hadi mpakani mwa Abel-mehola karibu na Tabathi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipozipiga zile tarumbeta 300, BWANA akafanya watu katika kambi yote kugeuziana upanga kila mmoja na mwenziwe. Jeshi likakimbia mpaka Beth-Shita kuelekea Serera hadi mpakani mwa Abel-Mehola karibu na Tabathi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipozipiga zile tarumbeta 300, bwana akafanya watu katika kambi yote kugeuziana upanga kila mmoja na mwenziwe. Jeshi likakimbia mpaka Beth-Shita kuelekea Serera hadi mpakani mwa Abel-Mehola karibu na Tabathi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakazipiga zile tarumbeta mia tatu, naye BWANA akaufanya upanga wa kila mtu uwe juu ya mwenziwe, na juu ya jeshi lote, jeshi likakimbia mpaka Bethshita, kuelekea Serera, hadi mpaka wa Abel-Mehola, karibu na Tabathi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Gideoni walipopiga tarumbeta zao 300, Mwenyezi-Mungu aliwafanya Wamidiani waanze kuuana wao kwa wao kambini. Waliosalia wakatoroka hadi Serera panapoelekea Beth-shita, hadi mpakani mwa Abel-mehola karibu na Tabathi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yale mabaragumu 300 yalipolia, Bwana akazielekeza panga zao wenyewe, kila mtu ampige mwenzake katika makambi yote; ndipo, hayo majeshi yalipokimbia mpaka Beti-Sita kunakoelekea Serera, wengine mpaka mto wa Abeli-Mehola karibu ya Tabati.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakazipiga zile tarumbeta mia tatu, naye BWANA akaufanya upanga wa kila mtu uwe juu ya mwenziwe, na juu ya jeshi lote, jeshi likakimbia mpaka Bethshita, kuendelea Serera, hata mpaka wa Abel-Mehola, karibu na Tabathi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Gideoni walipopiga baragumu zao mia tatu, Yawe akawafanya Wamidiani waanze kuuana wao kwa wao katika kambi. Waliobaki wakatoroka mpaka Zerera, wakafika Beti-Sita, hata kwenye mupaka wa Abeli-Mehola karibu na Tabati.